Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Leo nimesoma jibu la Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Pereila Ame Silima kwa swali la Mbunge wa Mheza Helbert Mtangi, kuhusu suala la uraia wa nchi mbili, nikaishia kuisikitikia sana Tanzania juu ya viongozi tulio nao. Mtangi kauliza juu ya serikali kuwa na kigugumizi kuhusu suala la uraia wa nchi mbili, na badala yake Naibu Waziri kaweka kigugumizi kibaya hata zaidi pale alipojibu ifuatavyo;
"Jambo hilo kwa sasa bado ni gumu lakini akataka wabunge kusubiri mchakato wa katiba mpya kama utaliweka kwenye orodha ya mambo yanayopaswa kuangaliwa"
Kwa mantiki hii ni kwamba Naibu Waziri, kwa niaba ya serikali, anasema kwamba;
Nimejiuliza sana, kuwa na Waziri katika serikali anaeweza kusimama mbele ya Wabunge, na kuutangazia umma wa Watanzania jibu kama hili, kwa swali ambalo wala halikuwa la nyongeza lenye kuhitaji jibu la kutoka kichwani.
Hivi hii nchi yetu ina tatizo gani la uongozi, ni kwamba tumekosa kabisa viongozi makini hadi tunafanya nchi yetu kuwa kama kichwa cha mwendawazimu ambacho tunataka kumjaribia kila mtu kuwa kiongozi?

- anaona utekelezaji wa uraia wa nchi mbili ni jambo gumu
- hajui hata kama suala la uraia wa nchi mbili litaingizwa kwenye orodha ya mambo yanayopaswa kuangaliwa
- hajui kama kama draft ya sasa ya katiba mpya inaongelea suala la uraia wa nchi mbili - ikimaanisha huenda hajui kwamba kuna hiyo draft ambayo tayari imeashatolewa rasmi na Tume ya Katiba