Mohammed Hamad
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 3,988
- 1,308
Habari zenu ndugu zangu wanajf,
Ni matumaini yangu waraka huu utawakuta mkiwa wazima wa afya ninyi na familia zenu.
Nianze na mkasa ulionikuta.
Jana majira ya saa tatu nilipita kituo cha kuandikisha vitambulisho vya uraia katika shule ya msingi Temeke jirani kabisa na msikiti wa Tungi. Nilionana na karani nikamuuliza mimi nina passport je wanataka copy nitoe kurasa zipi? yule bwana alinielekeza kuwa nitoe ukurasa wa kwanza kabisa ule ukurasa wenye maelezo mengi mengi na picha ya adam na amina/hawa/eva. Na ukurasa wenye details nilimuuliza kwanini nitoe ukurasa ule wa mwanzo ilhali ukurasa wenye picha una details zote? akaniambia ni lazima. Basi kwa kuwa ni lazima ilinilazimu nifanye vile nilivyoelekezwa.
Nikaenda kutoa kopi na kurudi kupanga foleni, ilipofika zamu yangu akawa ameingia bwana mmoja kutoka NIDA akasema watu wengine waende kwakwe kwaajili ya kuandikisha. Mimi nikaenda kwa yule yamaa nikasalimiana nae kisha nikampa kopi ta pasi yangu ya kusafiria akaniuliza huna kitambulisho chochote zaidi ya pasi ya kusafiria? nikamwambia ninavyo ila kwa kuwa tangazo linasema ukiwa na kimojawapo unaruhusiwa kujiandikisha ndio maana nikaenda na ile kopi ya pasi ya kusafiria. Akanijibu hapana sio kweli nenda kalete TIN, kadi ya mpiga kura na cheti cha kumaliza shule ya sekondari. Nikatoka na kwenda kuvichukua na kwakuwa nyumbani si mbali haikunichukua muda nikarudi tena.
Nilihakikisha nina vyeti mpaka vya chuo na transcripts ili nisije kukwazwa tena yaani nilijtahidi nina vyeti vya ziada na kopi zake.
Baada ya kurudi kuna mama mmoja akanstaajabu kuwa nimeweza kuwasilisha nyaraka zote kwa muda mfupi namna ile nakusema.
Mama: Yaani wewe mwelewa sana umeleta vyeti vyote sio kama hao wenzako wenye rangi kama wewe.
Mimi: Kwani mama wenye rangi kama mimi wanatakiwa kuja na vyeti vyote vilivyoorodheshwa kwenye fomu?
Mama: Ndio
Mimi: Kwanini? kwani sisi ni raia wa daraja la pili?
Mama: Sisi hatujui ila ndio maelekezo tulioelekezwa na bosi wetu.
Mimi: Nikamgeukia huyo bosi wao nikamuuliza kwanini anafanya vitu doble standards? kwanini anafanya mambo yanayomfanya ahisi kunyanyapaliwa na kutengwa kutokana na rangi ya ngozi yake? kwani kama ni mahitaji yawe ya siri wasitangaze kuwa Watanzania wenye asili ya asia waje na vyeti moja, mbili, tatu?
Nikamwambia hivi humu ndani mnaaminije kuwa hawa weusi hakuna wanaotoka msumbiji, rwanda, burundi, kongo na kenya? ukiwa mweusi hata ukienda na barua ya mwenyekiti wa serikali za mitaa unaandikishwa ukiwa mweupe unatakiwa uende na mlolongo wa vyeti.
Nadhani kuwa mweusi hakuamanishi wewe ni Mtanzania kwani Tanzania imezungukwa na nchi nyingi zenye watu wenye ngozi nyeusi ambao wanaweza kuchukua fursa hii adhimu kuupata uraia wa Tanzania kwa chee! Na nina sikia kuna vijana wengi wa kimsumbiji wapo hapa Dar wanafanya kazi za umachinga si ajabu hawa vijana kwa weusi wao wakaandikishwa na kuwa Watanzania lakini kuna weupe "wakuchovya" wakakataliwa kupata fursa hii kwa kuwa tu vyeti vilivyohitajika havikutimia.
Kwakuwa JF ni mahali wanapopita watu wa kadi mbalimbali naamini mtatoa ushauri na kuchukulia hili swala kwa uzito stahiki!
Mwisho ni ushauri mdogo kwa NIDA.
Msihangaike sana na Watanzania wenye asili ya asia wasiofika hata laki tano! Hangaikeni na Weusi wanaoweza kufikia nusu yetu aprox 40 mil. Pengine Watanzania tupo wachache sana ila hii kasumba ya kila mweusi ni Mtanzania ndio inayoongeza idadi inabidi kila mmoja afanyiwe upembuzi yakinifu wa vyeti vyake apewe uraia stahiki.
Wasalam.
Mohammed H. Shossi
P.O.Box 19181
Dar es Salaam, Tanzania.