KASALE MALETON MWAANA
New Member
- Jul 29, 2021
- 0
- 10
POMBE~Ni kinywaji kinachotengenezwa kwa kutumia mimea Kama ngano, mahindi, ndizi na mimea nyingine yenye sukari asilia ndani yake kwa njia ya uchachu ( fermentation process).
DAWA ZA KULEVYA~ Ni dawa zozote( zaweza kuwa za asili au za kutengenezwa kiwandani) ambazo mtu akitumia huchochea mfumo wa utendaji kazi wa mwili kwa namna moja ama nyingine.
URAIBU ( ADDICTION) ~Ni Ile Hali ambayo mtu hupenda kutumia kitu fulani zaidi kupindukia kiasi kwamba hawezi Tena kufanya kazi au kuishi kwa Amani bila kutumia kitu hicho. Ni ulevi usio wa kawaida ambapo mtumiaji wa kitu fulani hawezi kukaa kwa muda mrefu bila kutumia kitu husika au kufanya Jambo husika alilozoea kufanya kila siku.
URAIBU KATIKA MADAWA YA KULEVYA NA POMBE~ Ni hali ya mtu kuwa mtumiaji wa dawa za kulevya au Pombe, kwa kiasi kikubwa, ambayo hupelekea mabadiliko ya mfumo wa ufanyaji kazi wa mwili Kama mfumo wa fahamu ( nervous system) na mifumo mifumo mingine ya mwili kiasi kwamba mifumo hiyo haiwezi kufanya kazi yake vizuri mpaka mtu awe amepata dawa hiyo au Pombe.
Dawa hizo au Pombe huchochea mfumo wa mwili kufanya kazi kwa haraka kupita kawaida au kwa taratabu Sana kupita kawaida kulingana na aina ya dawa ya kulevya au Pombe.
Maswali ya msingi yanayoweza kusaidia kuelewa maana ya uraibu wa madawa ya kulevya na Pombe.
✓ kwa Nini paketi ya sigara huandikwa " uvutaji wa sigara Ni hatari kwa afya yako" na bado watu hununua sigara kwa wingi?
✓kwa Nini chupa za Pombe huandikwa " unywaji wa Pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako" na bado mtu huweza kutumia Pombe bila kujipimia kiasi Cha kutomdhuru?
Baada ya kujua maana ya pombe, dawa za kulevya na uraibu, hebu Sasa tuangazie madhara ya dawa za kulevya na Pombe katika jamii.
Kila kitu kikitumiwa kwa kupita kiasi huleta madhara. Pombe ukitumiwa kwa ustaarabu na kwa kiasi kinachokubalika na wataalamu haina madhara. Lakini kitu chochote kikitumika kupita kiasi huleta madhara.
(Too much is harmful)
MADHARA YA POMBE NA DAWA ZA KULEVYA KWA AFYA YA MTUMIAJI.
• pombe Kali husababisha vidonda vya tumbo ( stomach ulcers).
• matumizi ya pombe kupita kiasi husababisha magonjwa ya ini Kama homa ya ini ( liver cirrhosis) na magonjwa mengine ya ini pamoja na kufeli kwa figo ( renal impairment). Kumbuka kazi kubwa ya ini mawilini Ni kuchuja sumu na sumu hiyo kuondolewa nje ya mwili kupitia Figo. viungo hivyo nyeti vikiunguzwa na Pombe husababisha matatizo makubwa mwilini hata kupelekea kifo.
• sigara na dawa zingine zinazotokana na tumbaku zina kemikali inayoitwa nikotini ( nicotine) ambayo husababisha msukumo mkubwa wa damu( high blood pressure), mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida ( abnormal heartbeat), na matatizo mengine katika mfumi wa upumuaji na mfumo wa nzunguko wa damu.
•moshi ya sigara huathiri mfumo wa upumuaji kwa kusababisha magonjwa ya mapafu Kama bronchitis, saratani ya mapafu ( lung cancer) na magonjwa mengine ya mfumo wa upumuaji.
• madawa mengine ya kulevya Kama bangi na mirungi huathiri mfumo wa fahamu ( nervous system) hivyo hupelekea mtu kuwa katika Hali ya kutojifahamu au matatizo ya akili ( mental illness/ mental retardation).
•pombe pia huongeza sukari mwilini hasa kwa wagonjwa wa kisukari ( Diabetes patients). Hii Ni kwa sababu, Pombe inapoingia mwilini, mwili una tabia ya kutumia kwanza Pombe kuliko chakula nyingine Kama mbadala ya kutengeneza nishati ( energy in form of ATP) hivyo kufanya chakula kingine ndani ya mwili kuongeza kiwango Cha sukari mwilini.
YAFUATAYO NI MADHARA YA POMBE NA MADAWA YA KULEVYA KWA FAMILIA NA JAMII KWA UJUMLA
• uraibu wa Pombe na madawa ya kulevya huongeza umaskini kwa kuwa mtu hutumia hela nyingi na kununua dawa hizo na Pombe. Pia hukaa muda mrefu bila kuzalisha kitu chochote Cha faida
•uraibu wa madawa ya kulevya huchochea kuongezeka kwa uhalifu katika jamii. Hii Ni kwa sababu watumiaji wa madawa ya kulevya huweza kufanya Mambo mengi ya kihalifu kama ukabaji, ubakaji, uuaji n.k. kulingana na kwamba dawa au Pombe huathiri utimamu wa akili kiasi kwamba sio rahisi tena kujizuia kutojihusisha na uhalifu.
•kuongezeka kwa maambukizi ya magonjwa mbalimbali hasa magonjwa ya zinaa ( veneral diseases). Hii Ni kwa sababu watumiaji wengi wa madawa huweza kujihusisha na matendo maovu Kama ngono zembe na hata ubakaji Jambo ambalo hupelekea maambukizi ya magonjwa kuongezeka.
• kuongezeka kwa malumbano ya kifamilia na hata kuvunjika kwa ndoa nyingi.
NINI KIFANYIKE KUPUNGUZA MATUMIZI YA DAWA YA KULEVYA NA POMBE.
•Jamii wapewe elimu juu ya madhara ya Pombe na madawa ya kulevya katika afya zao na maisha ya kawaida
•Wanafunzi kufundishwa maadili mema na kuepuka kujiunga kwenye makundi mabaya ( peer pressure/ peer groups) ambayo hushawishi matumizi ya dawa za kulevya na Pombe.
•Serikali kuweka msisitizo katika kupiga marufuku dawa za kulevya nchini
•watumiaji wa Pombe kupewa elimu ya kiasi Cha Pombe kisichoweza kuleta madhara kwa siku.
•Viongozi wa dini kuendelea kuwa watu mafundisho ya dini yanaweza kuwafanya watu wengi kutojihusisha na unywaji wa Pombe na madawa ya kulevya.

Upvote
5