Naitwa Mundu nimezaliwa kwenye familia ya watoto saba. Baba yangu alifukuzwa kazi sababu ya ulevi na upinzani wa kisiasa mwaka 1996, mwaka mmoja tu baada ya mimi kuzaliwa nikiwa mtoto wa nne kati ya watoto saba.
Familia haikuwa na amani sana mwanzoni kwa sababu ya ulevi uliopindukia na msongo wa mawazo uliosababishwa na ukosefu wa kazi ambao ulimkumba baba yangu, kwa hiyo mzee akawa hawezi kuishi bila kulewa na wala hakujiusisha na shughuli yoyote ile ya kimaendeleo, ni yeye na pombe pombe na yeye. Watoto tukabaki kulelewa na kusomeshwa na mama yetu aliyekuwa mhudumu wa afya katika zahanati ya kijiji.
Maisha hayakuwa magumu sana kwa sababu ya jitihada ya mama kuipambania familia, namshukuru sana Mungu kwa ajili ya zawadi ya mama mpambanaji na ambaye hakukata tamaa. Mama yagu aliamini sana katika elimu na kuajiriwa kwa hiyo alitukazania sana kusoma masomo ya sayansi kama unavyojua ndio yanayoaminika kwenye nchi yetu kutoa ajira kwa asilimia kubwa hasa hasa masomo ya afya na ualimu wa masomo ya sayansi na pia kuepuka ulevi na makundi ya vijana ya migomo na upinzani wa siasa ili tusije ishia pabaya.
Basi nilivyokanyaga shule sikutia uvivu nikasoma haswa na kutia bidii kwenye masomo ili nije niiokoe familia yangu, nikafaulu vidato vyote na kupangiwa chuo kikuu mji mkuu wa kibiashara (Dar-es-salaam). Hapo ndipo akili ilipochanganyikiwa na kuchangamshwa na maisha ya watu na mambo ya jiji hili. Mama yangu alinikanya ulevi wa pombe, uraibu wa madawa na makundi ya vijana wa mjini, niliyatii mashauri hayo niliyohusiwa na mama mzazi. Lakini mtoto wa shambani mimi nikakutana na uraibu mpya ambao watu wengi hawaujui kwamba ni uraibu lakini wanautumia sana na wanautumia kama sehemu ya shughuli zao za kila siku na baadae kupitiliza na kuutumia kwa mambo mengine ambayo sio afya kwa akili, roho na miili yao.
Kama tunavyojua uraibu hutajwa kama ugonjwa (hasa wa afya ya akili) na utumwa wa kushindwa kutumia kitu pasipo kiasi au kujizuia kama vile pombe na madawa ya kulevya mfano tumbaku, bangi, kokaini, heroini na mengineyo. Watu wenyewe shida hii hupelekwa kwenye maeneo maalumu yenye wataalamu kuwasaidia kupunguza utegemezi wa vitu hivyo na kurudi katika hali ya kawaida. Lakini uraibu huu mpya umewapata watu wengi na hawafahamu kama wameathirika nao na mbaya zaidi hakuna msaada wowote ambao utawasaidia kujinasua na uraibu huu niliokutana nao.
Uraibu huu kwa bahati mbaya zaidi umeharibu watu wa rika zote kuanzia vijana wa mashuleni mpaka wazee bila huruma huku ukitumia kivuli chake cha faida nyingi, kumbe ni kama panya unang’ata na kupuliza.
Uraibu huu umegawanyika katika makundi makubwa matatu, ambayo yana faida chache kwa upande mmoja na hasara nyingi kwa upande mwingine kama nilivyotangulia kusema uraibu huu unang’ata na kupuliza. Uraibu huu mpya mimi Mundu niliokutana nao ni (uraibu wa teknologia ya mitandao) ambao umetukamata watu wengi katika maeneo makubwa matatu.
Uraibu wa picha na video za ngono; nikiwa chuoni mwaka wa kwanza ndipo nilipobahatika kununua simu janja yangu ya kwanza, nilichelewa kidogo ukilinganisha na watoto kutoka familia nyingine ambao humiliki simu hizi kuanzia kidato cha kwanza au pengine chini ya hapo. Kwahiyo ulimbukeni wa kuitumia ulikuwa mkubwa saana kushinda kwenye mitandao kuangalia kila kilichofunguka mbele yangu, nikawa navutiwa saana na watu wanavyovyaa kuishi na kujionyesha nikifikiria kuwa ni uhalisia wa maisha kumbe ni wachache saana ambao ni uhalisia na wengi wao ni maigizo tu.
Basi nikawa nasoma maoni ya watu wengine chini ya machapisho yao walioweka kwenye mitandao hiyo, cha ajabu kila baada ya maoni mawili matatu ya machapisho hayo kuna picha, matangazo au tovuti zilizokuwa zinakupeleka moja kwa moja kwenye picha na video za ngono, wadada kwa wakaka wakiuza na kununua miili yao kama soko la kimtandao.
Kilichoniuzunisha zaidi kuona mpaka vijana wa kiume na wenyewe katika karne hii wanauza miili yao kujipatia riziki inahuzunisha saana na kuumiza moyo wakati kwa mara ya kwanza ilizoeka ni wanawake ndio walikuwa wakiuza miili yao. Na bahati mbaya zaidi wanauza miili yao kwa kutumia matundu yao yote ya mwili, namaanisha mdomo, sehemu ya haja kubwa na haja ndogo kitu ambacho ni hatari sana kwa afya ya mwili na akili.
Haikuishia hapo tu kuweka matangazo kwenye maoni ya machapisho ya watu maarufu kwenye mitandao ya kijamii bali yametengenezwa mpaka makundi ya mitandao ya kijamii ambapo watu wamekusanywa humo wa rika zote na jinsia zote wakitangaziana na kununuana.
Kufanya hivi kila siku kunaleta hali ya mazoea ndani ya ubongo na fahamu za watu kwahiyo kila muda anatamani kuona na kufanya matendo haya ambayo kwa mara ya kwanza hayakuwepo katika jamii yetu. Kufanya hivi kunahitaji muda na pesa, pale pesa inapokosekana na tayari hali ya mazoea imeshajengeka kichwani (uraibu) ndipo tunaposikia mambo ya ubakaji watoto wadogo na urawiti wa vijana wetu.
Mambo haya yanafanywa na watu wa karibu yetu ambao tumewaamini na kuishi nao majumbani, kumbe hatufahamu tayari ni wagonjwa wa uraibu wa video na picha za ngono. Maana mtu hawezi akafanya jambo ambalo hajajifunza wala kuliona, ubakaji na urawiti ni matokeo yake pale watu wanapokosa sehemu ya kumalizia kiu za uraibu huu.
Tumeona watu mbali mbali hadi viongozi wakubwa wakikamatwa na kamera wakiwa wanaangalia picha na video hizi au ndugu zetu wa karibu kujikuta wakituma kwa kukosea. Mambo haya yanadhihirisha watu wengi waliotuzunguka tayari wana ugonjwa huu unaosambaa sana kama kirusi.
Kila uraibu huanza kama majaribio ya kutafuta furaha furani kwenye mwili ya mtu lakini kiakili mtu huyo huitaji kuacha uraibu huo. Ila kiu ya uraibu huizidi kiu ya kuacha kwahiyo hujikuta anarudia jambo ambalo akili haiitaki kila mara na kuwa kama sehemu ya maisha.
Je, tutafanyaje kuokoa jamii yetu na janga hili?

- Uraibu wa picha na video za ngono
- Uraibu wa mahusiano ya mitandaoni
- Uraibu wa michezo ya kubahatisha

Upvote
1