SoC04 Uraibu wa michezo ya bahati nasibu

Tanzania Tuitakayo competition threads

masabo94

New Member
Joined
Jun 20, 2024
Posts
1
Reaction score
6
STORY CHANGE YA URAIBU WA MICHEZO YA BAHATI NASIBU
Nguvu ya uchumi ndio sauti pekee katika Taifa lolote Duniani, hata hivyo wazalishaji wakuu wa uchumii ni vijana , kwa kutambua umuhimu wa vijana katika nguvu kazi ya uchumi Mataifa Mengi yameweka sera mbalimbali za kumuinua kijana katika ngazi uchumi.

Tanzania pamoja nakuweka mipango mbalimbali ya kumuinua kijana kiuchumi ikiwemo kuweka mikopo maalum kwa vijana,kuanzisha mafunzo wezeshaji kwa vitendo pamoja na kuhamashisha vijana wasome kwa bidii ili wafikie ndoto zao bado serikali imeacha Jini(mzimu) linalo angamiza na kutekeza vijana wa kizazi hiki linalojulikana kama URAIBU WA MICHEZO YA BAHATI NASIBU.

“Kilisikika kilio cha mwanaume mmoja akisema kamali!! Kamali!! kamali !! imenifanya nijute kuzaliwa kwani sasa natamani kufa kuliko kuishi mana imenifilisi kila nilichomiliki”.

Michezo ya bahati nasibu ni aina za michezo inayochezwa baina ya watu wawili yenye makubaliano ya fedha au kitu kwa atakayefanikiwa kushinda. Michezo hii inamajina mengi yakuvitia mteja kulingana na matakwa ya mmiliki au mwanzishaji .Aidha michezo hii imekuwa kwa kasi kubwa na yenye kuwavutia mamia ya vijana kutokana na namna ya upataji wa fedha wa haraka tena bila kutumia nguvu nyingi na jinsi inavyotangazwa kwenye vyombo vya habari,mitandao ya kijamii na kwa kutumia watu maaarufu wenye ushawishi kwa vijana.

Michezo hii inaendeshwa kwa ubunifu ,akili na mahesabu ya juu sana jambo ambalo vijana wengi hatujajua. Hata hivyo mara tu anavyojiunga au kuanza inakupa hamu ya kuendelea tena kucheza ukiamini ipo siku utashinda jambo linalopelekea uraiubu wa mchezo.

Kutokana na ushawishwi na uraibu wa michezo hii kumekuwa na ongezeko la wimbi kubwa la vijana wanaocheza katika ngazi zote za elimu,wafanyakazi,wajasiliamari, Maafisa wa serikali, bodaboda na machinga jambo ambalo linaathari kiuchumi,kijamii na kiafya.

Mafanikio ya mshindi mmoja katika michezo ya bahati nasibu kwa hasara ya mamia ya vijana hutuwezi kusema ni mafanikio ya kiuchumi bali ni anguko la uchumi kwa vijana, Tuko katika kizazi kisichopenda kufanya kazi kwa bidii , kuweka akiba ya fedha, kuingia katika ushindani wa kibiashara ili kujikwamua kiuchumi.

Michezo ya bahati nasibu ni kamali iliyoboreshwa ambayo inaendelea kuua fikra za vijana kwa kufurahia kile wanachopewa na si kile wanachopaswa kutengeneza cha kuwaingizia kipato cha kila siku ili waweze kupiga hatua.

Uhuru wa fedha ni sayansi kamili inayoongozwa na falsafa,kanuni na Taratibu yenye kuambatana na kufanya kazi kwa bidii pamoja na kuchagua maisha ya nidhamu katika mpangilio na utumiaji wa fedha ulio sahihi. Aidha uchumi Imara wa mtu huwa ni mchakato endelevu unaoweza chukua muda au kipindi fulani ambapo vijana wengi tunadhani unaweza lala maskini ukamka Tajiri.

Kutokana na changamoto au hasara katika utafutaji wa fedha ambao umeowakuta mamia ya vijana wengi baadhi yao wamejikuta wamekata tamaa za kuendelea mbele katika kufika uchumi wa juu na hivyo wanaamua kuingia katika michezo ya bahati nasibu bila kujua kila jambo zuri linagharama zake.

katika hatua ambayo inatisha na yahatari ni kuona sasa michezo hii ya kamali inachezwa na kupendwa na Watoto wa shule jambo ambalo si afya kwa Taifa kwani linateketeza kizazi kinachokuja.

Katika jitihada za kupinga michezo ya bahati nasibu nimekuwa mwanaharakati katika kuwashauri na kuwaonya vijana kuhusu madhara ya jambo hili lakini nimejikuta kama mpiga kelele masikioni mwa watu bila ya mafanikio yoyote tena nikijibiwa na baadhi ya watu kama serikali imekubali wewe ni nani?????


Kwasababu ya uraibu wa michezo ya bahati nasibu kwa vijana imepelekea madhara yafuatayo.
Kupungua kwa uwezo mkubwa wa kufikiri katika ngazi ya kiuchumi.waraibu wa michezo hii huwa wanakosa muda mwingi wa utulivu wa kutafakari mbinu au vyanzo vipya vya fedha kwa kuwa muda mwingi wanaupoteza kwenye kufuatilia michezo hiyo.

1. Kuharibika kwa Afya ya akili. Baadhi ya vijana wemejikuta wakiingia katika msongo wa mawazo kutokana na kupoteza vitu vya thamani hali ambayo inapelekea kukosa usingizi.

2. Migogoro ya familia, michezo hii imesababisha hata baaddhi ya ndoa nyingi kuvunjwa pia kutokuwa na maelewano mazuri kati ya ndugu na ndugu kwani jambo hili linakinzana na Imani za dini.

3. Kukosa nidhamu ya kuweka akiba. Kwasababu ya uraibu wa michezo kijana yuko tayari kutumia fedha alinayo au akiba yake ili akidhi nia ya kucheza.

4. Mauti, baadhi ya watu wamejikuta wakichukua maamuzi magumu ya kukatisha Maisha yao kutokana na msongo wa mawazo uliosababishwa na kufilisika na kupoteza vitu vya thamani.

5. Hivyo ili tuwe na Tanzania bora yenye uchumi imara lazima vijana tujikite katika uzalishaji mali na kufanya kazi kwa bidii na kuacha michezo ya bahati nasibu hivyo nashauri yafuatayo;

1. Kuacha michezo ya bahati nasibu kwani si njia sahihi ya kujikwamua kiuchumi.

2. Vijana tuamine katika uwezo tulionao kwani tukitumia ipasavyo tunafanikiwa.

3. Vijana tuingie kwenye ushindani wa kibiashara ili kujikomboa kiuchumi.

4. Vijana tusipende njia ya mkato kwenye uchumi kwani uchumi imara ni mchakato

5. Vijana tutumie muda katika uzalishaji na uwekezaji unaofaa kwa kufuata sharia za nchi.

6. Umoja wa vijana ngazi zote bila kujali itikadi za vyama ,kabila au dini kushinikiza serikali kufuta makampuni yote yanayojihusisha na biashara ya bahati nasibu pamoja na kutoa ushauri kwa vijana.

Mwisho

Natoa shukrani zangu kwa uongozi wa jamiiforums kwa kunipa fursa ya kutoa mawazo yangu kama kijana ili tuwe na Tanzania bora MUNGU awabariki sana.
 
Upvote 3
Nimesoma na maumivu sana kamari imeniaribia sana maisha yangu ila Leo ni rasmi sitaki Tena kujihusisha na aina yeyote ya kamari
 
Nimesoma na maumivu sana kamari imeniaribia sana maisha yangu ila Leo ni rasmi sitaki Tena kujihusisha na aina yeyote ya kamari
Tatizo la tabia ni mchakato mkubwa sana, Huwezi ukaamka asubuhi na kusema naacha tabia fulani .
 
acha kupangia watu namna ya kuishi! kila mtu ana mfumo wake wa kujipatia kipato. uraibu uko hata kwenye pombe, uzinzi, wizi, umalaya, ushoga, n.k ishi maisha yako, ya wengine achana nayo, hayakuhusu!
 
Betting inaenda kuaffect sehemu ya ubongo ambayo ni reward system kama drugs tu zilivo
inafanya inakuwa ngumu sana kuacha!
Watu wa kubet poleni sana!It takes an army to QUIT,Naelewa sababu i've dealt with drug addicts sana
 
mi apa nafungua account ya bet online ya pm bet....tena nacheza zile computer logarithm hela nayotumia kwa pombe kwa mwezi inazidi desel ya kwenye gari..bora niibetie iwe furaha yangu mdawa kujiburudisha...
 
mi apa nafungua account ya bet online ya pm bet....tena nacheza zile computer logarithm hela nayotumia kwa pombe kwa mwezi inazidi desel ya kwenye gari..bora niibetie iwe furaha yangu mdawa kujiburudisha...
hahahaaaaa nimepiga milion 43juzi kati kasheshe ipo kwenye kuzitoa zote, kila siku unatoa milioni 3 mafala sana hawa jamaa, nikajikuta nacheza tena nikaliwa karibu 10m ila zilizopona nimeopoa kwa siku 10 na nimefanyia kazi ya maana aisee hata kama wanatutafunaga nimewalamba kwenye zile jackport hot20
 
Hili ni janga la taifa kwa kweli serikali inatakiwa kuchukua hatua madhubuti kusitisha leseni za betting co. Magufuli aliona hili na alikuwa njian kupoteza makampuni ya betting nchin. Nimeona koment za baadhi ya vijana wakisema kila mtu ana njia yake ya utafutaji ni kweli lakn betting is not an option kabisa ya kuchagua, inapoteza focus ya mtu & Time na kufanya mtu kushindwa kufanya mambo ya msingi kwake yey binafs na kwa jamii kwa ujumla. Ninaushuhuda wa karibu sana wa washikaji wengi waliopoteza mwelekeo wa maisha kisa betting. kwa kijana anaeza betting hawezi elewa hiki kbs.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…