SoC01 Uraibu wa Ponografia

SoC01 Uraibu wa Ponografia

Stories of Change - 2021 Competition

Jade_

Senior Member
Joined
Apr 19, 2015
Posts
122
Reaction score
214
`Kuna mtu hapa Jamii Forum alielezea kisa chake na kwamba anaweza kujifungia ndani akiangalia video za ngono huku akipiga punyeto kwa masaa hata 12. Kuna watu walifikiri hii ni “chai” (uongo) lakini watu wanapata sana hizi shida ila hawawezi kuongea kwa kuwa ni aibu kwenye jamii. Unaweza kukuta kundi la vijana limeinamia simu ukafikiri wanafanya kitu cha maana kumbe wanaangalia ponografia. Siku hizi hata watoto wanakutana na hizi video mtandaoni na zinawaharibu mapema sana. Rejea uzi wangu wa jinsi mtoto anavyoathiriwa na elimu anayopata akiwa mdogo sana.

Watu wengi sana wameingia katika dimbwi la uraibu wa video za ngono za mtandaoni, na wanatafunwa taratibu bila wao wenyewe kujijua. Uraibu huu ni mbaya sana kuliko uraibu wa madawa au pombe na madhara yake ni kama ya kulevya. Familia zinaangamia, vizazi na vizazi hurithishana tabia hizi na watu wanabaki na maumivu makali sana kwenye nafsi zao. Rejea uzi wangu kuhusu uraibu wa ngono kiujumla. Uraibu huu unasababisha magonjwa mengi ya kisaikolojia kama vile sonona, kuharibu ubongo kibayolojia, kuumwa mwili na kwa wanaume zinapunguza nguvu za kiume na hata kupelekea uhanisi. Mtu atalalamika sana, atazunguka hospitali zote na kwa waganga wote kutafuta tiba ya ugonjwa wa nguvu za kiume lakini tiba inaweza kuwa kuacha kuangalia video za ngono. Uraibu huu unaambatana na uraibu wa kupiga punyeto.

Dalili za uraibu wa video za ngono ni kukaa muda mwingi sana mtandaoni unatafuta video hizi. Yaani kama upo nyumbani unaanza kwanza taratibu kusaka video ambazo zinaweza kukidhi mahitaji yako huku unapiga punyeto na ukikaribia kufikia mshindo unaacha kwanza unaendelea kutafuta video nyingine tena. Mwingine akiona tu tarakinishi tayari anapata hamu anatamani aende tu kwenye video hizo. Mtu kama huyu, kwa sababu waigizaji kwenye sinema hizi wanafanyia plastic surgery sehemu zao za siri (wanawake) na wanachukuliwa wale wenye maungo makubwa (wanaume) basi anatamani tu kulala na watu wa aina hii. Anakuwa hana hamu na watu wa kawaida, na kwa wanaume atajiona amepungukiwa nguvu za kiume.

Dalili nyingine ni kwamba mtu huyu anaanza kuwa na tamaa nyingine ambazo hakuwahi kuwa nazo kama vile mapenzi ya jinsia moja, kupitia mtaroni, mapenzi na watoto, mapenzi na wanyama au mapenzi na ndugu. Anataka kufanya staili za kila namna akiona kwenye video hizi na kifo cha mende kinaonekana ni ushamba. Hii ni kwa sababu ponografia hushtusha na hisia za kushtuka na za kupata hamu zinafanana sana (moyo unadunda kwa haraka zaidi, unaanza kusikia joto nk). Hivyo basi unaufundisha ubongo kwamba ili upate raha inabidi uangalie na kufanya makubwa zaidi vitakavyokushtua. Utaanza na video za ngono za kawaida lakini kadiri unavyoendelea kuzoea utatafuta zinazokushtua ambazo si za kawaida na mwishowe utajikuta ambako ukuwahi kutarajia kuwepo. Dalili zipo nyingi na chache za kuongezea ni mtu kupoteza mahusiano mazuri aliyowahi kuwa nayo kama ya ndugu jamaa na marafiki, kutokufanya vizuri shuleni na kazini, kubadilika hulka ghafla bila sababu ya msingi nk.

Video za ngono za mtandaoni kiukweli ni aina ya udhalilishaji kwa wanawake. Hata wanawake wanaocheza hizi video wanakuwa tayari wana matatizo ya kisaikolojia (aidha waliwahi kudhalilishwa kingono au walilelewa kwenye mazingira hatarishi) kwa hiyo wanakuwa na chuki binafsi. Mwanamke mwenye uraibu wa kuangalia video hizi atataka kufanyiwa kama wanawake kwenye hizi video wanavyofanyiwa (matendo ya aibu) na bila ya yeye kudhalilishwa anaona kama hajapata raha.

Kwa wanaume wao ni mwendo wakudhalilisha. Asilimia kubwa ya video kwenye tovuti za ponografia zinahamasisha kutoka na watoto, kutoka na ndugu, kufanya mapenzi ya jinsia moja, kubaka, kufanya unyanyasaji wa kingono nk. Hii inajionyesha moja kwa moja kwenye jamii, mtu anaona kama kumvunjia au kuvunjiwa heshima ndio mapenzi yenyewe. Kitu ambacho si kweli na husababishia watu vidonda visivyotibika.

Kama una uraibu huu lazima ufanye kila namna uache kuangalia video za ngono. Kufanya hivi ni ngumu mno lakini ni kitu kinachowezekana. Kama mtu anavyoanza kuacha madawa ni lazima kwanza uanze kupunguza kuangalia video hizi. Siku za mwanzoni utajisikia vibaya sana, unaweza hata kuumwa lakini ni muhimu ujikaze na usikate tamaa. Unatakiwa kupunguza taratibu mpaka uje kuacha kabisa.

Wewe mwenyewe utashangaa jinsi maisha yako yatakavyobadilika na pia hata matatizo madogo (kuumwa, uchovu, kukosa hamu ya kula, kutoweza kufikiri au kutumia ubongo kwa kina nk.) yatapotea kwenye maisha yako. Watu wengi wanafikiria kwamba wamelogwa lakini yote haya ni madhara ya ponografia. Video za ngono si za kuangalia mara mojamoja, bali ni kitu cha kutoangalia kabisa.

Kitabu cha Your Brain on Porn: Internet Pornography and the Emerging Science of Addiction cha Gary Wilson kinaongelea kwa ukubwa na kwa undani zaidi kuhusu uraibu huu.
 
Upvote 41
Porn na Punyeto huwa zina roho chafu ya kishetani, ukishafnya kitendo hiki pepo hao huuanza kufanya kazi yao na dalili ni kukosa amani, kukosa hamu ya kuishi, kujihisi hauna thamani . Kuna video nyingi Youtube zinaonesha pepo hao wakitolewa kwa maombi.

Jinsi ya Kuacha ni kumfanya Yesu kuwa role model wako. Kumbuka hakuna kitu chochote kinaweza kukupa furaha katika hii dunia.

Furaha ya kweli ipo kwenye kusali na kujazwa Roho Mtakatifu rohoni mwako. Pombe , Uzinifu zina furaha ya muda na maumivu makali ya muda mrefu. STAY PURE. - MWILI NI BOKSI LA ROHO, NA WEWE NI ROHO
 
Porn na Punyeto huwa zina roho chafu ya kishetani, ukishafnya kitendo hiki pepo hao huuanza kufanya kazi yao na dalili ni kukosa amani, kukosa hamu ya kuishi, kujihisi hauna thamani . Kuna video nyingi Youtube zinaonesha pepo hao wakitolewa kwa maomb...
Kabisa. Kila mtu amshike Mungu wake labda anaweza kumsaidia.
 
Porn na Punyeto huwa zina roho chafu ya kishetani, ukishafnya kitendo hiki pepo hao huuanza kufanya kazi yao na dalili ni kukosa amani, kukosa hamu ya kuishi, kujihisi hauna thamani . Kuna video nyingi Youtube zinaonesha pepo hao wakitolewa kwa maombi...
Umeongea Vyema kabisa yaani katika kuishinda punyeto au kuanagalia pornography ni kumruhusu Yesu
Sasa kuna wengine anakwambia fanya mazoezi ya mwili ,mara usikae peke yako peke yako mda mrefu hii haiwezi saidia sisi ambao tulishawai ku experience tunajua kbs kuwa ni Yesu pekee ndo anaweza komesha
 
`Kuna mtu hapa Jamii Forum alielezea kisa chake na kwamba anaweza kujifungia ndani akiangalia video za ngono huku akipiga punyeto kwa masaa hata 12...
"kuharibu ubongo kibayolojia, kuumwa mwili na kwa wanaume zinapunguza nguvu za kiume na hata kupelekea uhanisi"

☝☝☝☝ unaweza kufafanua zaidi?
 
Ni kweli kabisa, inaua sana uwezo wa binadamu wa kufikiri kwa kina na mambo ya maana...

Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
"kuharibu ubongo kibayolojia, kuumwa mwili na kwa wanaume zinapunguza nguvu za kiume na hata kupelekea uhanisi"

☝☝☝☝ unaweza kufafanua zaidi?
Ubongo unaharibika kwa kupungua "grey matter". Watu wakiangalia porn grey matter inapungua na wakiacha grey matter inarudi.
Wanaume wanapungukiwa nguvu za kiume kwasababu kuangalia porn inawapunguzia sana hamu ya kufanya ngono na wanawake wa kawaida.
Pia kupiga sana punyeto kuna chosha sana mifumo ya uzazi ya wanaume hivo kupunguza kabisa uwezo wao wakuproduce sperm kwa ufanisi.
 
Asante sana kwa andiko zuri.

I have ever been a victim ya huu ushetani. Eeh Mungu baba unirehemu mimi mkosaji. Lakini namshukuru sana kwa neema yake alinitoa huko katika hilo shimo la kuzimu. Tukimruhusu Mungu atubadilishe anafanya.

Mpaka leo namuomba sana sitaki rudi kule. Everything kiliharibika nikapoteza dira ya maisha. I always wanted to die 😢😢😢. Lakini huyu Yesu aliponitoa jamani jamani.

Nawaombea wote waliokamatwa wafunguke wakaachiliwe kutoka huko. Neema yake Bwana Yesu ikawaangazie mkapate nuru yake. Mungu baba watetee wote wanaotamani kupona na adui.

Its possible. If you want let us pray together ili Bwana akatutee tutoke huku. PM for help jinsi ya kutoka huku. Its not easy. Bwana Yesu mwenyewe atahusika na atatusaidia. Shetani mbaya sana.
 
Katika vitu vilinipa shida kuviacha ni punyeto, nilanza 2015 nikaaza kuacha 2019 nilipamua kuishi na mwanamke imenipa tabu maana hata baada ya Kuwa na mwanamke bado ilikuwa ilinisukuma kupiga hivi ninavyoongea last time kupiga ni mwaka Jana mwishoni Hadi leo sijapiga Tena na ninaweza kujicontrol kabisa, Mwanzo nilikuwa siwezi ila Sasa nadhani Pepo limeamua kusepa.
 
Back
Top Bottom