MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 843
Leo kuna mdau hapa JF kasema kitu ikanifanya nifikirie hili swala. Je ikatokea chama kimoja kika shika serikali na kingine kikawa na idadi kubwa zaidi ya wabunge ina faida? Mimi naona hapa yatatokea moja kati ya haya.
1. Kutakuwa na uwiano mzuri wa madaraka yani checks and balances. Kwa maana hiyo chama kinaacho shikiria serikali haiweza kufanya ndivyo sivyo ikijua wabunge wao wata pitisha tu agenda yoyote watakayo ipeleka bungeni. Kwa maana hiyo hapa itailazima serikali kupeleka hoja bungeni ambazo zinaonekana wazi ni kwa manufaa ya taifa ambalo bunge lenyewe ni lazima lipitishe.
2. Shughulu za serikali zitasimama na uendeshaji wa serikali utakuwa wa tabu zaidi. Kwa maana hiyo kunakuwa na deadlock. Hii itatokana kama chama chenye wabunge wengi zaidi kikiamua kususia hoja mbali mbali za serikali makusudi ili serikali ionekana imeshindwa kutimiza wajibu wake.
Swali langu ni je kama hali hii ikitokea Tanzania lipi kati ya haya mawili lina nafasi kubwa la kutokea? Kwa hali yetu ya kisiasa je itatokea sababu namba moja au itatokea sababu namba mbili? Je kuna uwezekano wa kutokea scenerio tofauti na hizi mbili? Ni scenerio ipi hiyo nyingine inayoweza kutokea?