Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Urais ni siku zote ni kubeba majukumu, Urais ni uwajibikaji, Urais nikutoa huduma kwa watu. Hakuna namna Urais utakosa kutupiwa lawama hata kama utafanya mazuri mengi kiasi gani.
Tatizo la Tanzania tumeondoka kwenye principles za Urais tumekeza kupambana na ukosoaji bila kujua hata Rais anaposimama jukwaa lazima akosoe wenzake. Hakuna siku Rais amewahi kutoa hotuba bila kukosoa wasaidizi wake, kukosoa wapinzani wake nk. Kama yeye anakosoa na wakati mwingine kuwatumbua wasaidizi wake kwa utendaji mbovu kwanini watendaji wake walazimishe kutokukosolewa. Leo Simbachawene ni Waziri lakini kesho anaweza kutumbuliwa kwa utendaji mbaya, Ni Nani atakayesema Simbachawene afanyi vizuri Kama si wananchi? Je, wakitaka kumkosoa Waziri watatumia njia gani Kama siyo vyombo vya habari na mitandao ya kijamii? Je, kwa mfumo huu wa Sasa Kama tutakamata wanaomkosoa Waziri nakuwafanya wahalifu tutasema wamehatarisha amani? Yaani kusema Waziri hafai ndo imekuwa kuhatarisha amani?
Lakini anateuliwa Waziri badala aeleze vipaombele vyake kwenye wizara yeye anakimbilia kukemea vyombo vya habari. Kimuundo Waziri Hana jukumu lakufundisha vyombo vya habari vifanyaje kazi, jukumu lake nikutatua changamoto za wizara. Siku chombo Cha habari kikikosea kitawajibishwa kwa mujibu wa sheria. Waziri amevikuta vyombo vya habari vipo ajaviunda yeye, wakati vinasajiliwa vilipewa sheria vikasoma na nakuelewa na watendaji wa vyombo hivyo wanajua mipaka yao. Waziri ateuliwi kuja kuvifundisha vyombo namna yakutoa huduma anateuliwa kwenda kutoa utatizi wa changamoto.
Mawaziri kuacha majukumu yao nakupambana zaidi na watu ndipo kunapelekea watumbuliwe lakini pia kila siku Rais Kama taasisi atazidi kukosolewa kwa sababu badala wasaidizi wake watatue changamoto zinazowakabili wananchi wao wanapambana na watu walioelimika na walioshiba wanaokaa mitandaoni Kuandika. Siku zote wenye njaa na ambao ndio tumepewa jukumu lakuwalisha Awana muda wakiandika mitandaoni, wanaoandika mitandaoni Ni wasomi na wanajua sheria inasemaje. Kibaya zaidi mahabussu hapaogopeki Tena ,hivyo kuangaika na matajiri na wanasiasa ukaacha kuwahudumia wananchi nikumfelisha Mhe. Rais.