Urais unachosha, ila ni mzuri. Rais Samia akituachia katiba mpya akastaafu 2025 itampa heshima yeye na kizazi chake kuliko kutuachia katiba baada 2025

Urais unachosha, ila ni mzuri. Rais Samia akituachia katiba mpya akastaafu 2025 itampa heshima yeye na kizazi chake kuliko kutuachia katiba baada 2025

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Nitaeleza Kwa kifupi faida za Mhe. Rais kutuachia katiba awamu yake ya Kwanza then akastaafu Kwa heshimu

1. Tayari amaeshakuwa Rais na hakuna Jambo jipya analoweza kulipata kwenye urais hata aliongoza miaka Mia.

2. Endapo ataamua kuingia kwenye uchaguzi 2025 Ndipo mchakato wa katiba uanze itamlazimu atumie mbinu zisizo za Haki kurejea madarakani yeye,wabunge na madawani kwani Hana uhakika kama anaoishi nao NI kweli niwafuasi wake au niwafuasi wa urais wake? Anao uhakika mmoja Tu WA mfumo wa dola.

3. Endapo atachafuka kwenye uchaguzi 2025 hata katiba atakayoleta itakuwa katiba yenye kutanguliwa na maridhiano mapya kutokana na machungu ya 2025 na hivyo kuondoa Imani aliyojenga Kwa wananchi sasa

4. Katiba itakayotafutwa baada ya 2025 itabidi aisimamie kupitia dola isijeikakisamabaratisha chama cha mapinduzi 2025. Kwa tafsiri nyingine katiba hiyo utamfanya awe WA Kwanza kuikiuka kuelekea kukabidhi nchi Kwa Rais mpya 2030.

5. Endapo ataamua kuiruhusu mchakato na kuukamilisha 2025-2030 na akataka uchaguzi wa yeye kukabidhi madaraka uwe WA Haki itamlazimu akubali pia misukumo ya kisiasa yakukiacha chama kikiwa na makundi na mgawanyiko mkubwa kwani tunaamini moja ya Jambo linalopiganiwa kwenye katiba nikumpunguzia Rais madaraka, means yeye baada ya katiba atakuwa na watu wachache wanaotegemea fadhila na nguvu yake kupata nafasi ya uongozi.

Kwa uchambuzi huu na Kwa mustakabali mwema wake na familia yake, afanye maamuzi yakuwa Rais WA awamu moja, aliyeiachia nchi katiba mpya, mfumo mpya wa utumishi, mfumo mpya wa kuendesha serikali na kufanya siasa.

Maamuzi haya Yana thamani kubwa Sana kuliko yeye kurudi kwenye ulingo WA kisiasa 2025 nakuvunja Yale aliyoeleza juzi.

Akirudi majukwaani anakwenda kupambana na kizazi ambacho shida Yao kubwa siyo madarasa, siyo elimu, siyo barabara, siyo maji n.k Bali shida yao kubwa ni mfumo bora wakuwafanya wao na familia zao kupata fursa ya keki ya Taifa baada ya kuona nchi inaelekea kumilikiwa na familia flani flani tu.

Natamani Mhe. SSH angeona faida yakutokurudi Kwa wananchi kuomba Kura akaamu kupambana na maendeleo pamoja na katiba na kukabidhi nchi yenye mfumo mpya Kwa watu wengine 2025.

Nakupenda Mhe. SSH na nakuombea Sana uyafikie malengo uliyotumwa na Mwenyenzi Mungu kuyafanya hapa Duniani. Ningependa uishi miyoyoni mwa watu kama anavyoishi Mwalimu Nyerere. Katiba inatosha kukufanya uishi miyoyo mwa wajukuu wa Taifa letu na Dunia Kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom