Urais wa Donald Trump 2024-2028 utakuwaje kwa Dunia na Marekani?

Urais wa Donald Trump 2024-2028 utakuwaje kwa Dunia na Marekani?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Ni wazi huyu bwana ameishashinda Urais wa Marekani na anasubiri tu kupitishwa na kuapishwa hapo mwezi January. Kulingana na sera zake urais wake utakuwaje kwa Marekani na Dunia? Baadhi ya sera zake kubwa ni.

1. Kuongeza kodi kwa bidhaa kutoka China kwa asilimia 60
2. Kuongeza kodi kutoka mataifa mengine kwa asilimia kati ya 10-20
3. Kudeport mamilioni ya wahamiaji haramu.
4. Atasimamisha sheria zinazohusiana na utunzaji na mazingira
5. Atafanya mabadiliko makubwa kwenye uchumi na kumuweka RFK Jr kuwa Kiranja wa masuala ya afya.
6. Kuongeza nafasi za kuteuliwa kwenye utumishi wa umma
7. Kufanya mabadiliko makubwa kwenye sera za elimu.
8. Kuwa bahili kwa Ukraine na Members wa NATO.
 
Nichukue nafasi hii kuipongeza serikali ya awamu ya sita inayo ongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha kuwa Donald Trump anakuwa Rais wa Marekani kwa kipindi cha miaka minne ijayo hakika hili lisingewezekana bila ya uthubutu wa jemedari wetu mkuu Samia Suluhu Hassan na naimani atahakikisha kuwa uchaguzi wa marekani unamalizika kwa amani.
 
Back
Top Bottom