TLS is a professional body na siyo kigenge cha wanasiasa kama ambavyo wewe unafikiria kichwani kwako. Ile taasisi inaendeshwa kwa sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali siyo matakwa ya Raisi wa TLS kama ambavyo wanasiasa mnavyoamua kuendesha siasa za UVCCM na BAVICHA.
Pili, TLS ina chapters: Unazifahamu hata chapters wewe ??? Hivyo siyo lazima wote twende Arusha kuchagua Raisi. Hizi Chapters zinasaidia mambo mbalimbali ya wanasheria na jamii yote kwa ujumla, hasahasa utoaji wa bora wa haki na utawala bora wa sheria.
Tatu, TLS ina vyombo vyake vya kimaamuzi kama Annual General Meeting (AGM) ambavyo vina nguvu. Raisi wa TLS kazi yake ni kusimamia miongozo yote ambayo inatolewa na AGM hivyo hajiamulii tu, kama wewe ambavyo unataka aamue. Kile ni chombo cha kitaalamu (A Professional Body) siyo cha kisiasa, japo mara chache hufanya shughuli za kisiasa kwasababu haziepukiki.
Nne, dunia nzima kuanzia Uingereza Raisi wa The Law Society of England and Wales hukaa madarakani kwa mwaka mmoja tu. Raisi huwa kama CEO akifuata maelekezo ya AGM, na hajiamuliii tu vitu vyake kama wewe unavyofikiria kichwani mwako.
.....Kabla hujatushauri sisi wanasheria kuhusu sheria nakushauri kasome kwanza sheria......
Wewe Layman kutaka kutushauri sisi Professionals on how to do our jobs properly it's similar to lowly Spartan trying to teach Ares (The god of war) basic combat skills. It's total abalone and a monkey business....
STOP IT BEFORE YOU EMBARRASS YOURSELF, TLS siyo BAVICHA au UVCCM..