Uchaguzi 2020 Urais wa Zanzibar hauuzwi bali ni kwa ajili ya Wananchi wa Unguja na Pemba

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar balozi Idd Seif amesema urais wa Zanzibar hauuuzwi bali upo kwa ajili ya wananchi wa Unguja na Pemba.

Balozi Idd ametoa onyo kwa wote waliojipanga kutumia rushwa ili kununua uongozi na kwamba wazanzibar watampendekeza Rais wanayemtaka kabla ya kupitishwa na vikao vya juu vya chama.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Jiwe limerushwa gizani hilo .. yoyote atakutana nalo
 
Rais wa Zanzibar miaka yote anateuliwa Dodoma, mwambie atulizane.
 
Toka lini waunguja na wapemba wakateuwa mgombea urais wa Zanzibar?
Wasubiri kuletewa toka chimwaga.
 
Aache kuwadanganya wenzake.

Rais wa mkoa wa Zanzibar tunamteua pale Dodoma Tanganyika, mambo ya kupiga kura ni kukamilisha formalities tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…