TEAM 666
JF-Expert Member
- Dec 7, 2017
- 4,399
- 8,594
LURAKOZE Shane Tanzania Saido Ntizabazonkiza. Ni Kirundi kinachomaanisha karibu sana Tanzania. Namkaribisha staa mpya wa Yanga.
Hii ndiyo Tanzania na yuko katika jiji ambalo Mkuu wake wa Mkoa sio staa sana kama zamani. Abuubakar Kunenge amepoa, lakini Dar es Salam yake imechangamka. Karibu Saidoo. - Saidoo ni fundi na nusu wa mpira.
Mafundi wa mpira huwa wanaheshimiwa sana nchini, kuna muda huwa wanaishi kama wanawake warembo wanaomilikiwa na matajiri. Huwa wananata.
-Alichokifanya Saidoo pale Arusha ajiandae na vitu vitatu muhimu kwa sasa. Kwanza kutembezwa katika maduka ya GSM kununuliwa bidhaa, pili kila boss wa Yanga, GSM atataka kupiga nae picha na kuzunguka nae katika gari ya kifahari, tatu ambacho ni kibaya, ataanza kuwindwa na wasichana warembo.
Atatongozwa. - Ataishi maisha haya. Hili nimuhakikishie, lakini raha atakazopata sasa ajue kuna kitu amekifanya, akiacha kufanya kitu hicho raha zitahamia kwa mchezaji mwingine. Mabosi wa mpira sio wanafiki. - Emmanuel Okwi alishajua kuishi na watu wa nchini. Hawakuwahi kumsumbua.
Nina mengi ya kumuandikia Saido, lakini kiufupi amuheshimu kila mtu, lakini asimuamini kila mtu. Akiishi katika mstari huo atakuwa na kesho nzuri Yanga. - Kuna mastaa walikuja nchini na ustaa wao kama sasa ilivyo kwa Saidoo, baadae wakasahau kilichowaleta, baada ya muda wakawa wa kawaida.
Saidoo ajichunge sana. Kama akiona kuna uzito amuulize Mrundi mwenzake Didier Kavumbagu kuhusu Dar es Salam na Tanzania. - Kavumbagu aliyekuja nchini, sio aliyeoondoka nchini. aliyekuja alikuwa moto Siku va kwanza namuona 2012 alizibariki nyasi za Uwanja wa Mkapa (Zamani Taifa) akiwa na jezi za Club Atletico kwa kuwafunga Yanga mabao mawili, baada ya mechi wa Yanga waliivamia kambi ya Atletico kutaka kumsajili na wakafanikiwa.
Kavumbagu akawa mali ya Yanga. Ndani ya Yanga akaanzia pale alipoishia Atletico. Mtaani hakujakalika, magazetini ndiyo usiseme. Kila Mwanayanga aliamini wamepata mtu wa kuwasaidia kwa muda mrefu. Kilichokuja kutokea baada ya kuizoea Tanzania na Dar es Salaam ni historia.