Hii habari inaonekana kuna ukweli ndani yake, leo asubuh TBC taifa walimuhoji Prof. Lipumba akaelezea liyoyaelezea, na baadae Gabriel Zakaria (mtangazaji) akmuhoji mkuu wa mkoa wa Tabora Abeid Mnyimusa kuhusiana na ukweli wa habari hizo. Mkuu wa mkoa akazungumzia point km 3 hivi. 1: Anadaia ni wavamizi ktk hifadhi, 2: waliouwawa ni wahalifu waliojificha huko si wapinzani kwani wanafanya uhalifu kwingineko na wanaenda kujificha huko porini. 3: Hakuna nyumba iliyochomwa moto, ila vibanda vya hao wavamizi ndio vilivyochomwa moto.
Mwandishi alipomuuliza km waliouwawa ni wapinzani kuna ukweli upi hapo? akang'ang'ania kusema ni wahalifu waliojificha ndani ya hifadhi.
Wito alioutoa prof. lipumba wa kutaka uchunguzi huru ufanyike una nafasi kubwa zaidi km ni kweli tunastahili kuitwa nchi ya demokrasia na yenye utawala bora wa sheria.
Mhalifu hauwawi anakamatwa na kupelekwa mahakamani, na mahakama ndio itathibitisha uhalifu wake na hukumu yake anayostahili kulingana na makosa aliyofanya.
Asasi huru za kisheria nchini na za kimataifa ziende eneo la tukio zifanye uchunguzi wao na kutupatia matokeo halisi yasiyochakachuliwa!!!