Urasimu unavyokimbiza wawekezaji nchini

Urasimu unavyokimbiza wawekezaji nchini

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
Maendeleo ni zaidi ya kutegemea katika kufanya mambo yako peke yako. Dunia ya leo inaelekeza kwenye social capital kuliko ilivyokuwa miaka kadhaa iliyopita.

Taifa haliwezi kuendelea likiwa huku likisukuma wawekezaji badala ya kuweka mazingira mazuri ya kufanya kazi kwa pamoja "mutual cooperation" na mataifa mengine.

Kila taifa leo linajenga mazingira mazuri ya uhusiano na mataifa mengine kwa kuhakikisha urasimu unapungua au unaondolewa kabisa.

Katika hali isiyofurahisha makampuni makubwa matano ya Volkswagen yanatarajia kuhamisha uwekezaji wake Tanzania na kuhamisha Rwanda kutokana na urasimu uliozidi Tanzania.

Kuna haja ya kuitathmini kauli mbiu yetu ya "Tanzania ya viwanda" na muono wa Taifa juu ya hatua tunazopiga.
 
Back
Top Bottom