Urembo bandia nusura uniletee mauti

Urembo bandia nusura uniletee mauti

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
150114125045_urembo__304x304_bbc_nocredit.jpg

Baada ya masaibu ya kujitakia urembo bandia, Urach hawezi tena kutembea kwani kwa sasa anatumia kiti cha magurudumu

Mwanamke aliyemaliza katika nafasi ya pili ya mashindano ya urembo amesema kupenda sana kujiweka urembo bandia nusura umletee mauti yake.

Andressa Urach alimaliza wa pili katika mashindano ya urembo ambapo mashabiki walimpigia mwanamke waliyehisi kuwa na makalio mazuri zaidi katika nchi yao kupitia kwenye mtandao wa internet.

Ili kujiongeza urembo, Urach aliambia jarida la Daily Mail la Uingereza kwamba alidungwa sindano za kemikali ili kufanya makalio yake kuwa makubwa pamoja na kuongeza ukubwa wa miguu yake.

Lakini mnamo mwaka 2013, mwili wake ulianza kuoza ndani.

Athari za kujiweka urembo bandia zilianza kumwandama wakati Urachhadi madaktari wakalazimika kutoa kemikali hizo kutoka mwilini mwake mwezi Novemba kwa kuchimba mashimo katika mapaja yake.

Mwili wake ilipatwa na mshtuko kwa sababu ya ugonjwa alioupata kwa kutumia vifaa chafu vya matibabu mwilini mwake.

150114125325_urembo__304x304_bbc_nocredit.jpg

Madaktari wametoa kemikali za sumu mwilini mwa Urach

Daktari mmoja wa kurekebisha na kutibu athari zinazotokana na urembo bandia alisema ugonjwa aliopuata Urach ulitokana vifaa chafu.

Madaktari hata hivyo waliweza kuokoa maisha yake lakini hadi leo anatumia tu kiti cha magurudumu na miguu yake ina mashimo mwengi ambayo madaktari waliweza kutoboa ili kutoa kemikali zenye sumu alizotumia kuongeza ukubwa wa makalio na miguu.

''Ninalipia makosa yangu leo kwa sababu nilitaka urembo kwa kila hali, ili nionekane kuwa kamili. Mungu ananiadhibu'' Urach aliambia Mail.

''Lakini badala ya kujiongeza urembo, niliharibu mwili wangu na sasa hata hauna sura.''

150114125214_urembo__304x171_bbc_nocredit.jpg

Urach anasema Mungu alimpiga kiboko kwa kujaribu kujibadilisha mwili wake kwa sababu ya kujitakia umaarufu

Urach pia alisema kwamba alikuwa na mazoea mabaya ya kufanyiwa uapasuaji wa kujiongeza urembo bandia kila alipojihisi kufanya hivyo.

''Sikuwahi kutafakari mara mbili wakati nilipokuwa nafanyiwa upasuaji lakini watu waliponionya nilidhani tu nitaweza kukabiliana na athari za hayo baadaye. '' Ningeweza kwenda kwa daktari, kama mfano nilivyozoea kwenda dukani na kuchagua nilichokitaka.

Nilitaka watu wanitazame na kusema tu , ''wow''

Kwa sasa Urach amejitwika mzigo wa kuwatahadharisha wanawake wengine kuhusu hatari za urembo bandia.


Chanzo: BBC

Sasa hivi bibie Urach kawa mzuri kuliko alivyokuwa mwanzo sasa hivi kawa kilema mzuri.
 
akome kabisa na bado wanawake wetu wa dar hawasikii kabisa.
 
Bado hawa wa kwetu yakiwakuta ndio watatia akili vichwani
 
Mnatusimanga sana na sony wega. Mie natafuta mkorogo kwanza niwe half caste
 
poor desperate girl...enlarging ''masaburi'' to gain attention...now thats reality check..
 
Bora nibakie hivi hivi cheusi mangala na uflat screen wangu hayo ya kemikali siyawezi
 
Halafu maimartha jesse anauza mapodozi ya kuongeza makalio..sijui kwanini hakamatwi na anajitangaza live
 
Back
Top Bottom