Urembo wa Ngozi, nywele na Kucha

Urembo wa Ngozi, nywele na Kucha

Kamanda Kazi

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2012
Posts
2,613
Reaction score
795
acne.jpeg

Urembo wa Ngozi, nywele na Kucha
Namshukuru Mungu Muumba Mbingu na Nchi kwa kutuweka hai hata leo. Yeye tu apaswa kutukuzwa na kuabudiwa!

Katika mfululizo wa post zangu nitaeleza kuhusu urembo wa ngozi, nywele na kucha ikiwa ni pamoja na namna ya kukufanya uonekane mrembo (kwa wanawake) na maridadi (kwa wanaume) ingawa mara nyingi wanaume hatujali sana mambo ya mwonekano mzuri wa ngozi, nywele au kucha zetu

Tutaanza na Ngozi.

Kuna mambo mengi ya kueleza kuhusu ngozi za miili yetu lakini nitagusia machache maana siwezi kumwaga kila kitu hapa jamvini. Hebu jiangalie ngozi yako jinsi inavyoonekana. Mwonekano wake unavutia ama la?

Mwonekano wa ngozi yako ni taswira au akisi (reflection) ya jinsi ulivyo kiafya ndani ya mwili wako! Mara nyingi tumejitahidi sana kuondoa magonjwa/matatizo ya ngozi kwa kupaka dawa katika ngozi. Yumkini tukaonekana tumepona lakini baada ya muda tena ile hali inajirudia! Tunatafuta dawa nyingine mbadala lakini matokeo ni yaleyale.

Mwonekano usioridhisha wa ngozi yako ni matokeo ya mwili wako kuwa na taka sumu (toxins) ambazo huziba tissues za mwili wako na kupelekea mwili kuwa na madoa au dosari/ugonjwa wa ngozi. Pengine utajiuliza sasa nifanye nini ngozi yangu iwe na mwonekano mzuri wa kuvutia.

Hebu fanya yafuatayo:-

1. Kula vyakula vinavyoleta na kuboresha afya ya ngozi. Vyakula hivi ni pamoja na dark orange beta carotene-rich foods' kama vile karoti, maboga, viazi vitamu, na magimbi. Apples, parachichi, maharage ya soya, shayiri, na yogurt na mboga za majani kama vile cabbage na spinach. Kula samaki kama vile dagaa, salmon, tuna, bluefish na monkfish. Tumia mafuta ya mizeituni katika saladi.

2. Epuka au punguza ulaji wa vyakula vilivyokaangwa (Fried foods), refined carbohydrates, vyakula vya ngano, nyanya, matunda aina ya machungwa na grapefruits, chocolate, strawberries, karanga na bidhaa yake (peanut butter) na vyakula vyenye mafuta mengi.

3. Epuka kula kupita kiasi (Overeating). Hii hufanya damu nyingi kusukumwa kwenda tumboni ili kusaidia uyeyushaji wa chakula hivyo ngozi kukosa supply' ya kutosha ya damu. Hali hii huikosesha ngozi viini rishe (nutrients) katka kiwango kinachotakiwa.

4. Kunywa juisi ya karoti, beet, celery, spinach na tango ili kuleta mng'aro wa ngozi.

5. Usikose kunywa angalau lita 3 za maji salama kila siku. Unaweza kukamulia limao au ndimu katika maji kwani itasaidia damu kutembea vizuri mwilini.

6. Kuwa makini na unywaji wa vinywaji vyenye kilevi (alcohol), vinywaji baridi (soda) zenye caffeine na kahawa kwa kuwa hupunguza kiasi cha maji katika mwili (dehydrate your skin).

7. Vaa nguo zilizotengenezwa kwa nyuzi za asili kama vile pamba.

8. Kila siku jipumzishe (relax) angalau kwa dakika kumi (10) ukiwa mtupu yaani bila nguo yoyote mwilini (Air baths). Hewa ya asili ni dawa ya ngozi ya bure kutoka kwa Lord God!

9. Fanya mazoezi ya viungo. Husaidia kutoa uchafu mwilini kwa njia ya ngozi. Pia huzalisha joto ambalo huua bacteria wenye madhara waliopo katika ngozi.

Kwa kuhitimisha mada kwa leo (ila tutaendela next time tukijaliwa uzima) nakufunza kutengeneza Chai ya Kichina iitwayo Chinese Cherry Tea.

Chai hii inywe mara kwa mara, itafanya ngozi yako iwe ya kupendeza na kuwa kama kijana! Hii chai husaidia ini, figo na utumbo kufanya kazi zake ipasavyo katika kuchuja na kuondoa taka sumu mwilini mwako. Chai hii ina vitamin A, B na C, na madini ya calcium, magnesium, potesium na chuma.

Vitamin A hufanya ngozi kuwa nyororo yenye afya isiyo na madoa. Vitamin B ina-balance kazi za ngozi na mfumo wa fahamu hivyo kuongeza uwezo wa kuhimili stress. Vitamin C hujenga collagen na elastin inayofanya ngozi yako isiwe na makunyanzi (wrinkles).

Chukua asali (kijiko cha chai), cherry jam isiyo na sukari (kijiko cha chai) na juisi ya limao (vijiko viwili vya chai) weka kwenye maji ya moto 300ml (chupa ya soda). Kunywa ikiwa bado moto! Mambo ndio hayo.

Kwa wenye matatizo ya ngozi kama vile acne, pimples, nk. Na kwa wale wanaopenda kuelekezwa jinsi ya kutengeneza vipodozi vya asili. (Next time nitaeleza madhara ya vipodozi vya viwandani).

Tuwasiliane
Simu 0688308840 au Email: alex.peter_75@yahoo.com
 
Back
Top Bottom