Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Serikali ya Ureno imepanga kuzinduzi sarafu mpya, CR7 Euro kumuenzi mfungaji bora wa timu yao ya taifa, Cristiano Ronaldo. Sarafu hii itakuwa ni ishara ya kuthamini mchango mkubwa wa Ronaldo kwa taifa la Ureno.
Cristiano Ronaldo ndiye mfungaji wa muda wote wa timu ya taifa ya Ureno, akiwa amefunga mabao 130. Uwepo wake umezalisha mafanikio makubwa kwa taifa, ikiwa ni pamoja na kuiongoza Ureno kwenye ushindi wa kihistoria wa Euro mwaka 2016 na kutwaa taji la UEFA Nations League katika msimu wa 2018/19.
Sarafu ya CR7 Euro inatarajiwa kuwa heshima kubwa kwa mchezaji huyu maarufu ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika soka la kimataifa.