Eng Kahigwa
JF-Expert Member
- Feb 18, 2014
- 783
- 631
Habarini wanaJF
Leo ninataka kutoa mada yangu kuhusu vijana (bado hawajaanza kujitegemea) hususani ambao hutegemea urithi kutoka kwa wazazi wao. Nimekuwa nikiona baadhi yao kutokuwa makini na maandalizi ya maisha yao hususani masomo na mengineyo, hii ni kutokana na kujipa ujiko kuwa kwa nini wajiandae kwa sasa wakati kila kitu kipo kinawasubiria, ambapo sio kitu chema; kwahiyo ni vyema ukajiandaa kwa kila litakalotokea mbeleni, maana huwezi jua kesho itakuwaje...labda kama mipango hiyo ikibadilika itakuwaje?
Kwanza kabla sijaanza kuelezea hilo jambo; kuna wazazi ambao uwezo wao ni mkubwa mno ambao huwapa vijana wao (ambao hawajaanza kujitegemea) kiasi kikubwa cha fedha, hilo sio jambo baya kwa mzazi kumfanyia kijana wake, ila kijana kama kijana unahitaji uone mbele zaidi katika maisha yako. Ni vyema kwa kijana ukajua jinsi ya kuitenga hiko kiasi cha pesa kwa asilimia flani ambayo unaweza kuzigawanya kama vile za matumizi, dharura na pia za kuwekeza. Hiyo pesa huweza ikakufanya uanzishe hata biashara yako ambayo itaweza kukuingizia kipato.
Kuhusu matumizi ni vyema kwa kijana ukaondoa vitu visivyokuwa na msingi hasa katika kutumia pesa. Chochote ulichokipanga ukakinunue ni vyema ukaenda moja kwa moja na sio kuangalia vya pembeni, nikimaanisha kukwepa na vitu viwezavyo kukuteka akili na kuitumia pesa yako bila kuwa na mpango huo. Na pia, ni vyema kijana ukajipangia kiasi cha kukitumia ndani ya muda flani ili kutoharibu bajeti uliyojipangia.
Nikija sasa katika mada yangu kuu; kwa kijana anayetegemea urithi kutoka kwa wazazi wao ni vyema kama akaangalia future ya maisha yake itakavyokuwa endapo atakuwa akiziendesha urithi huo. Vitu vya kuzingatia ambao baadhi yake ni Elimu na Kipaji ulichojariwa na Mungu muumba wako.
ELIMU: Kijana unabidi kama ni kusoma, usome kwa bidii na sio kujipa moyo kwamba urithi upo wa kukufanya uishi vizuri. Elimu husaidia pale utakapokubidi kuuendesha urithi huo, maana bila ya elimu usitegemee kama utaweza kuendeleza kuzalisha na kuendeleza mafanikio yako kupitia urithi huo, la sivyo utakuwa umepoteza kila kitu na usiwe na wa kumlaumu, na hata ukiomba siku zirudi nyuma ili utengeneze vizuri maisha yako...usitegemee kujibiwa, maana utakuwa umecheza na shillingi katika shimo la choo.
KIPAJI: Kipaji humsaidia mtu hata kwa yule sliye na asiye na elimu. Vipaji huwa vinaweza vikawa kama vile; uongozi, michezo, kujua kazi kwa kipindi kifupi na pia kuwa na hekima. Ukiwa na kipaji cha uongozi na ukichanganya na hekima, ni rahisi sana kuongoza makampuni, taasisi na mambo mengine ya kuongeza kipato.
Natumai kila mmoja wetu atakuwa ameelewa mambo baadhi yanayohusu hii mada niliyoielezea.