SoC02 Urithi wa Mwanangu

SoC02 Urithi wa Mwanangu

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Jul 26, 2022
Posts
1
Reaction score
1
Kijana wangu Sasa umekuwa si mtoto tena, umeingia umri wa kuyajenga, umri wa majukumu, natamani ningekufundisha haya ana Kwa ana ila muda Sio Rafiki hivyo nimekuandikia walaka huu utakaokusaidia katika Safari Yako kama ukizingatia Lazima utafanikiwa.Hekima na Busara zangu zitakupa muongozo na kuongeza maarifa.

Haya ni Mambo 8 muhimu ya kuzingatia Ili upate kufanikiwa÷

MAADILI
vijana wa sasa mnaona haya mambo ni kama ya wazee wazamani, na ndio maana watu wengi wanaishia kuumia na ukiangalia utandawazi umeharibu maadili hivyo kuna mmomonyoko mkubwa sana wa maadili. Kisicho sahihi kwa sasa watu wamekifanya ni sahihi, na hakuna anae ongea kuhusu hili. Ila yatunze maadili yako, maana matendo yako ni mbegu kijana wangu, na lazima utavuna tu yale uliyo yapanda. Jipende, jiheshimu, jitnze, jiwekee mipaka na jilinde. Haya yatakufanya kuwa bora Zaidi na kupata uwezo wa kujidhibiti maana kitu kikizidi hugeuka kuwa sumu, hivyo ni lazima ujue nyakati ulizopo, kipi unafanya na kwa wakati gani. Maadili yatakulinda kila unapotaka kuteleza na mambo ya duniani.

UADILIFU
Hili ni jambo muhimu sana katika safari yako ya mafanikio. Vijana wengi hawana Uadilifu ni waongo Hadi katika kazi hawana muaminifu iwe katika kazi na mahusiano pia. Vijana wengi hawafiki mbali kwasababu wana ukosefu wa Uadilifu utakufanya uweze kudhibiti mihemko, kuwa mwenye nidhamu, kujiheshimu, mwaminifu, nadhifu, msimamo pamoja na maamuzi thabiti. Hii itafanya watu wengi wakuamini na itakusaidia kuonekana na Watu na hata kukupa vyeo,mamlaka n.k

HESHIMA
Muheshimu kila mtu awe mkubwa, awe mdogo maana Baraka za mtu zipo kwa mtu. Usijivunie, usijikweze na ondoa kiburi. Kumbuka kua utu duniani ni wa muhimu na hakuna aliye bora kuliko mwenzake. Tume umbwa kutegemeana na kusaidiana na ndio maana aliyenacho yule wewe hauna, na ulicho nacho wewe yule hana. Hivyo usimdharau usie mjua maana huwezi jua kesho ukianguka ni nani atakuokota, au ukishindwa nani atakae kuinua. Maisha ni vita hivyo tunaitaji watu mbali mbali ili kusudi tuweze kuishinda vita hii.

MAARIFA
Usiache kujifunza maana elimu haina mwisho na maarifa yana letwa na elimu pamoja na ujuzi. Na hili kuongeza hekima na busara, ni lazima ukubali kufundishwa sababu sio kila jambo unalijua, hivyo unapokutana na mtu au watu kuwa mnyenyekevu upate kujifunza kila kitu ambacho hauna. Maarifa yata kufungulia milango mingi ya mafanikio yako.

UPENDO
Ndio kitu pekee kinacho tutofautisha kati ya binadamu na wanyama, hivyo hakikisha una upendo wa kweli kwa watu wanaokuzunguka. Upendo wa kweli unaleta Amani, furaha, msamaha, huruma, upole na ukweli. Hivyo katika safari yako unahitaji maana hii itakufanya uwe mnyenyekevu kwa watu wote na utaweza kuwasaidia wengine. Jua unapopewa madaraka, vyeo, mamlaka jua siyo kwaajiri yako bali kwaajili ya watu wanaokuzunguka. Hivyo katika Baraka ulizojaliwa hakikisha pia unawabariki wengine ili mwenyezi Mungu azidi kukubariki, na kukupa kila hitaji la moyo wako.

MTAZAMO
Niamini ili ndilo tatizo la kwanza ambalo inabidi ulikabili, maana kitu chochote Ili kionekane kizuri au kibaya,kidogo au kikubwa kinatokana na mtazamo wako wewe. Huu ndio unaoweza kukujenga au kukubomoa. Kua na mtazamo chanya hata katikati ya magumu, maana ugumu wa kitu unaanzia katika mtazamo wako, jinsi unavyolipokea na kulitafsiri katika kichwa chako. Tatizo sio tatizo ila ni vile wewe unavyo chukulia kuwa tatizo ndio ukubwa wa tatizo unavyokuwa. Chagua kuona Baraka katika kila laana, wepesi katika kila ugumu, uzuri katika kila baya na wema katika ubaya. Ukiwa na mtazamo chanya basi muda mwingi utapata utulivulu wa kuamua lililo jema katika kila changamoto unayopitia. Ukibadili mtazamo wako katika kulielekea jambo au wakati unapo pambana na changamoto zako basi ni rahisi sana wewe kushinda katika kila changamoto.

MUDA
Wakati ni rasilimali pekee ambayo ikienda Haiwezi kurudi, hivyo chunga sana muda wako na ukiwa duniani hapa maana muda wetu unakikomo. Hakikisha unautumia muda wako vizuri ili usije ukawa na majuto. Wakati ni pesa, wakati ni ukuta. Hivyo ukitaka kufanikiwa hakikisha linalowezekana leo lisingoje kesho. Mambo ya leo yafanye leo maana leo ni siku pekee yenye uhalisia, kesho ni fumbo ambalo hatuwezi kulifumbua sisi wanadamu. Jua kutofautisha nyakati na jambo lipi lifanyike je muda wako mwingi unaupoteza kwenye nini? Je, unafaidikaje na muda huo? Ukitaka kuwa na mafanikio makubwa basi heshimu muda na hii itakufunza kujiwekea mipaka ni kipi ufanye na kwa muda gani, watu wapi uwe nao kwa wakati upi na kipi kifanyike kwa wakati upi? Jambo hili litakufanya uweze kujidhibiti na utajikuta huna hata muda wa kufanya mambo ya ajabu na kupoteza muda. Ujana ni maji ya moto, ujana ni kipindi cha kuyajenga na kutatua changamoto zako ili uishi vizuri hivyo angalia unapoteza muda wako wapi na kwa kufanya nini na unafaidikaje.

UWEPO WA MUNGU
Mwenyezi mungu yupo na ndio muumbaji wa hii dunia na mbingu, na vitu vyote vinavyo ishi ndani ya dunia hii ikiwemo mimi na wewe. Hivyo yakupasa umtegemee Mungu kwa akili zako zote, uwezo wako wote, na kwa nguvu zako zote ili uweze kufanikisha mambo mengi. Na ili uweze kutekeleza yote hayo basi ni lazima umjumuishe mwenyezi Mungu katika kila mipango yako ili ushindi uwe upande wako. Hii ndiyo point ya muhimu kuliko zote hapo juu lakini nimeiweka mwisho ili ujue huwezi kukamilisha yote hayo pasipo kuwa na Mungu ndani yako, una muhitaji Zaidi ili upate kushinda yote.

Maisha ni vita kila siku tunayo amka tunakwenda katika mapambano, tuna pambana kuishi, kutatua changamoto na kukamilisha malengo. Maombi na neno. La Mungu ni nyenzo muhimu sana katika safari yako ya ushindi lakini ili uweze kuyashinda yote kwa kishindo, mfanye Mungu awe silaha yako kuu ni yeye Mungu wa miungu, Baba wa mababa, Mwalimu wa waalimu, Fundi wa mafundi, Mungu wa vita, Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya duniani na mbinguni. Hii itakufanya uwe na hofu ndani yako na utajiwekea mipaka maana uwepo wa mungu katiaka maisha yetu ndio kitu pekee kinacho tutofautisha binadamu na wanyama wengine. Pasipo na mungu ndani yetu tunageuka na kua wanyama mfano mzuri angalia katika jamii zetu watu wanavyo ishi sasa hawana tofauti na wanyama. Hakikisha Unatumikia yeye atupae uhai.

HITIMISHO
Ishi maisha yako kama unakufa kesho, na fanya mambo yako yafaayo kama vile utaishi milele. Natumaini haya machache yatakusaidia katika safari ya maisha yako ya mafanikio. Sifa zao usiziweke kichwani na maoni yao usiyaweke moyoni.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom