Urusi imefanya jaribio la kombora la nuclear

Urusi imefanya jaribio la kombora la nuclear

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Russia imefanya jaribio la kombora la nuclear, ambalo Rais wa Nchi hiyo, Vladmir Putin amesema kwamba litawafanya maadui wao kuacha kuwafikiria.

Jaribio hilo limefanyika miezi miwili tangu Russia ilipoivamia Ukraine.

Putin alionekana kwenye televisheni akiambiwa na wakuu wa jeshi kwamba kombora hilo la masafa marefu limefanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza.

Jaribio limefanyika kutoka Plesetsk, Kaskazini Magharibi mwa Russia na limepiga malengo katika Penisula ya Kamchatka, umbali wa karibu kilomita 6,000.

Jaribio hilo la kombora hata hivyo halikushutua Nchi za Magharibi, lakini limefanyika wakati kuna mivutano mikubwa ya kisiasa.

Russia haijadhibithi mji wowote mkubwa wa Ukraine tangu ilipotuma maelfu ya wanajeshi wake Nchini Ukraine, Februari 24, 2022.

Source: Aljazeera

===

Sarmat: Russian missile will make enemies think twice, says Putin

Russia successfully tested the Sarmat intercontinental ballistic missile (ICBM) with President Vladimir Putin boasting the nuclear-capable projectile will make Moscow’s enemies “think twice”.

Putin was shown on television being told by the military the missile had been launched from Plesetsk in Russia’s northwest and hit targets in the Kamchatka peninsula in the far east on Wednesday.

“I congratulate you on the successful launch of the Sarmat intercontinental ballistic missile,” Putin told the army in televised remarks.

“This truly unique weapon will strengthen the combat potential of our armed forces, reliably ensure the security of Russia from external threats, and make those who – in the heat of aggressive rhetoric – try to threaten our country think twice.”
 
Huyu ni mpuuzi, kwani Nato hawana nuclear arsenals kama zake? anajuaje kama wao hawana tena zaidi yake?
Vita ya nuclear sio simple kihivyo kiasi cha kufanyia show off au piga nikupige kama manati na mawe.
Madhara ya nuclear ni world ending mostly the collapse of modern civilization na worst case scenario ni extinction.
Hata huku Africa tutahusika na madhara yake na hao NATO hawatakuwa na cha kufanya zaidi ya kukaa kimya tu sababu wanajua aftermath.

Putin anachofanya ni suicide attempt na dunia nzima ni mkubali au tufe wote.
 
Ataziona siku akianza yeye,kama kinachompata sasa hivi huko Ukraine kwa silaha ambazo alikuwa hazijui
Wakianzisha piga nikupige ya nuclear basi hakuna atakayemuona mwenzie.
Nuclear sio mchezo wa mieleka.
 
Huyu ni mpuuzi, kwani Nato hawana nuclear arsenals kama zake? anajuaje kama wao hawana tena zaidi yake?
We acha maneno ya kwenye khanga hebu thibitisha kama una huo ubavu nakuruhusu tumia vyombo vyote vikiwamo VOA, CNN, BBC, REUTERS, n.k
 
Moto wa Zelensky si mchezo, andunje anafikiri mkwala wa kutest nyuklia utamzua Zelensky kutembeza kisago, andunje anajidanganya sana kichapo kipo pale pale.
 
Hizo Nuclear sio peke yake alionazo Mungu atunusuru na mwendawazimu.
 
Urusi ina majigambo ya kiduanzi,kama mpaka leo imeishindwa UKRAINE, NATO wataiweza wapi?🤔
 
Back
Top Bottom