Urusi waonesha ubabe wa kijeshi ili kuwadhibiti NATO

Urusi waonesha ubabe wa kijeshi ili kuwadhibiti NATO

Mr.Black

Member
Joined
Jun 9, 2014
Posts
97
Reaction score
74
Habari wa jf katika hali inayoonesha kuwa Raisi wa urusi kwa sasa anahakikisha kurudisha heshima na nguvu ya Urusi ulimwenguni , siku za karibuni ameendeleza mazoezi makali ya kijeshi nchini humo


Uraisi wa urusi Vladimir Putin ametoa amri kwa jeshi la urusi mazoezi makali ambapo kundi kubwa la jeshi la taifa hilo kubwa duniani limefanya mazoezi ma mpakani mwa Taifa hilo hasa maeneo ya kusini , magharibi mwa taifa hilo .


Raisi ametoa amri kujibu mapigo kutoka mataifa ya magharibi , ambapo vikosi vya jeshi la NATO wakifanya mazoezi makubwa eneo la Balkan yakijumuisha vikosi vya majeshi zaidi ya 2,000 kutoka mataifa 14 vimefanya mazoezi hayo mazito kijeshi mpakani mwa Urusi . pia kwa upande mwingine majeshi hayo yamekuwa yanatuma vifaa vya kijeshi kwenda nchi ya Georgia iliyovamiwa na Urusi mwaka 2008

kwa mujibu wa Dr Konstantin Sikov amesema kuongezeka kwa mafunzo makali ya kijeshi kwa kipindi cha miaka 3 ni kutokana na kuongezeka kwa hali ya wasi wasi dunian hasa katika majeshi na hivyo wao kama viongozi wa wana wajibu wa kuchukua hatua kuweza kukabiliana na hali hiyo , akitolea mfano uturuki kuingia vitani nchini syria na muda huo huo marekani wakiunda makundi mipakani mwa Taifa hilo .
Sergei Shoigu ambaye amekuwa waziri wa ulinzi wa Urusi tokea 2012 amehamasisha idara ya mambo ya kivita ya urusi kurudisha mfumo wa kufanya ukaguzi wa kushitukiza katika jeshi la urusi ili kuweza kujua kama jeshi hilo linakuwa tayari kwa vita muda wowote ikitokea
kwa kipindi cha zaidi ya miaka 3 Jeshi la urusi wamefanya mazoezi ya kijeshi mara 20 , pia kwa mujibu wa Raisi wa Academy ya Geopolitical Problems anasema mazoezi ya kijeshi ambayo Raisi putin ameanzisha ni mazoezi ambayo ni ya kiwango cha juu na hayajawahi kutokea
pia colonel Leonid Ivashov amesema kuwa ana uhakika kuwa mazoezi hayo ni makubwa na kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu , wajibu wa vikosi vya majeshi ya Taifa limebadilika haraka kwa sababu ya kuongezeka hatari za kiusalama dhidi ya taifa lao ambazo hatari hizo zinaweza kukwamisha na jeshi na vyombo vingine vya kiusalama vya taifa hilo

Ameongeza kuwa hata Raisi Putin anaenda vikosi vya jeshi la taifa hilo ni kutokana na matendo ya Mataifa ya Magharibi kuweka dunia hali ya ukorofi wa kivita kutokana na matendo ya mataifa hayo yanayoendelea kufanywa hasa katika mipaka ya taifa hilo na wao wana wajibu wa kuhakikisha ulinzi na usalama wa taifa hilo.
 

Attachments

  • Vladimir-Putin-Russia-war-704067.jpg
    Vladimir-Putin-Russia-war-704067.jpg
    29 KB · Views: 180
  • 155962.jpg
    155962.jpg
    71 KB · Views: 121
  • 155963.jpg
    155963.jpg
    58.7 KB · Views: 113
  • 155967.jpg
    155967.jpg
    68.4 KB · Views: 122
  • 155969.jpg
    155969.jpg
    74.9 KB · Views: 119
  • 155971.jpg
    155971.jpg
    62 KB · Views: 136
  • 155972.jpg
    155972.jpg
    47.8 KB · Views: 113
  • 155973.jpg
    155973.jpg
    64.6 KB · Views: 115
  • 155974.jpg
    155974.jpg
    34.5 KB · Views: 108
  • 155975.jpg
    155975.jpg
    35 KB · Views: 138
  • 155976.jpg
    155976.jpg
    70.1 KB · Views: 115
  • 155977.jpg
    155977.jpg
    67.7 KB · Views: 108
  • 155978.jpg
    155978.jpg
    70.8 KB · Views: 119
  • 155979.jpg
    155979.jpg
    36.2 KB · Views: 112
  • 155980.jpg
    155980.jpg
    31.3 KB · Views: 110
  • 175817.jpg
    175817.jpg
    46.7 KB · Views: 110
  • 175818.jpg
    175818.jpg
    33.2 KB · Views: 131
  • 175819.jpg
    175819.jpg
    82.4 KB · Views: 111
  • 175820.jpg
    175820.jpg
    89 KB · Views: 111
  • 175821.jpg
    175821.jpg
    51.4 KB · Views: 328
Wengine wamekazania kufanya mazoezi ya kuvunja matofali kwa kutumia kifua tu, jamaa naona wanajiandaa na Warsaw pact hao NATO wajipange na ubepari wao
 
Yaani mnashangaa mazoezi jeshini?
Mimi sioni cha kushangaa hapo.
 
Nampenda sana Putin kwa jinsi anavyopambana na hawa Illuminati kuiokoa dunia. NATO ni mpango maalum wa Illuminati kuingiza agenda zao katika dunia.
 
Nampenda sana Putin kwa jinsi anavyopambana na hawa Illuminati kuiokoa dunia. NATO ni mpango maalum wa Illuminati kuingiza agenda zao katika dunia.
NATO,USA na RUSIA ni dugu 1 na wana lengo 1 wanatuigizia tu kutupumbaza.
Kumbuka uhalisia si halisi mkuu.

form1
 
Back
Top Bottom