Urusi yafanya mashambulizi makubwa ya anga nchini Ukraine

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Urusi imeendesha wimbi kubwa la mashambulizi ya anga dhidi ya Ukraine usiku wa kuamkia Jumapili na kusababisha kifo cha mtu mmoja huku wengine saba wakijeruhiwa.

ayo yameelezwa leo na mamlaka za Ukraine zilizobaini kuwa aliyeuawa ni rubani wa ndege ya kivita chapa F-16. Yuriy Ihnat, mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha jeshi la anga la Ukraine, amesema shambulio hilo lilikuwa kubwa zaidi kwa kuwa Urusi ilitumia silaha za kurushwa kutokea angani zipatazo 537 ikiwemo droni 477 na makombora 60. Jeshi la Ukraine limesema limefanikiwa kudungua 249 huku zingine 226 zilipoteza mwelekeo.

Hayo yanajiri wakati siku ya Ijumaa, rais wa Urusi Vladimir Putin alisema kuwa tayari kwa awamu nyingine ya mazungumzo ya amani mjini Istanbul, lakini kuongezeka kwa mashambulizi hayo ya mabomu kunafifisha zaidi matumaini ya kufikia mafanikio katika juhudi za kuvimaliza vita hivyo vilivyodumu kwa miaka mitatu na kusababisha maafa makubwa.
 
Very inefficient! Wanatumia silaha 537 kuua mtu mmoja?
 
Jeshi la Ukraine pamoja na Zelezesky ni waongo sana - hawana zana za kutungua ndege na Drones kiasi hicho,vita hii imekwisha washinda we sema ni vig'an'ganizi!!
 

Mashambulizi Makubwa ya anga, kafa mtu mmoja na 7 kujeruhiwa ( Sijaelewa maana naaahambulizi Makubwa ya anga vs Mazara yake )
 
Very inefficient! Wanatumia silaha 537 kuua mtu mmoja?
Mkuu usiamini propaganda za Zelensky na jeshi lake, jamaa hawa waongo Sana, sasa kama wana uwezo mkubwa WA kutungua ndege na Drones nyingi za Urusi kwa nini Zelensky huwa anamsubuwa subuwa Trump akiomba msaada WA air defense systems - si anasema anajiweza sana,sasa kulikoni??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…