Urusi yakanusha tuhuma za kumsaidia Trump

Urusi yakanusha tuhuma za kumsaidia Trump

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289
Urusi imeyaelezea madai ya idara za upelelezi za Marekani kuwa Rais Vladimir Putin huenda alisimamia juhudi za kujaribu kumsaidia Donald Trump katika uchaguzi wa Marekani wa 2020 kuwa yasiyo na msingi.

download-8.jpeg

Ripoti ya ujasusi ya Marekani iliyotolewa jana imeongeza maelezo mengine kwenye tuhuma kuwa baadhi ya maafisa waandamizi wa Trump walijaribu kushirikiana na Urusi kwa kusisitiza madai yaliyotolewa dhidi ya aliyekuwa wakati huo mgombea Joe Biden na viongozi wa Ukraine wenye mahusiano na Urusi kuelekea uchaguzi wa Novemba 3.

Ubalozi wa Urusi nchini Marekani umesema katika taarifa kuwa waraka uliotayarishwa na idara ya ujasusi ya Marekani ni tuhuma nyingine zisizo na msingi dhidi ya Urusi kwa kuingilia michakato ya kisiasa ya ndani ya Marekani.

Imesema hakuna maelezo na ushahidi uliotolewa kuthibitisha tuhuma hizo. Duru tatu zimesema kuwa Marekani inatarajiwa kuiwekea vikwazo Urusi katika siku chache zijazo kwa sababu ya tuhuma hizo.
 
Back
Top Bottom