Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Polisi ya Urusi imemkamata Dmitry Gudkov mmoja ya wakosoaji wakubwa wa ikulu ya Kremlin na taarifa zinasema huenda atakabiliwa na kifungo jela.
Taarifa za kukamatwa kwa Gudkov zimethibitishwa na baba yake mzazi aliyesema kuwa alikamatwa baada ya msako wa polisi kwa madai ya kutolipa kodi ya nyumba tangu mwaka 2015.
Baba wa Gudkov, aitwaye Gennady aliandika kupitia ukurasa wa Twitter taarifa za kukamatwa kwa mwanaye akisema kundi la watu waovu limekamata hatamu za uongozi nchini Urusi na linawatesa watu wa kawaida.
Mapema jana polisi ilifanya upekezi kwenye makaazi ya Gudkov yaliyopo nje kidogo ya mji wa Moscow pamoja na kwenye nyumba za ndugu na jamaa wa mkosoaji huyo.
Ikiwa atapatikana na hatia ya madai hayo ya kukwepa kodi, Gudkov anaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 5 gerezani.
DW Swahili