HERY HERNHO
Senior Member
- Mar 4, 2022
- 110
- 458
Mapigano katika mji wa Mashariki mwa Ukraine wa Bakhmut ambayo ni ngome muhimu, yanaongezeka na Rais Volodymyr Zelensky anasema hali huko inazidi kuwa mbaya.
Rais huyo anasema wanajeshi wa Urusi wanaharibu chochote ambacho Waukraine wanaweza kutumia kama ngao. Anasema wameendelea bila huruma, lakini majeshi yake hayajakata tamaa.
Wakati huo huo, Urusi inasema inakabiliwa na mashambulizi nchini mwao. Gavana wa eneo la Moscow alisema droni ilianguka katika mji wa Kolomna. Katika ujumbe uliotumwa kwenye mitandao ya kijamii, alidai kuwa miundombinu ya kiraia imekuwa ikilengwa.
Rais Vladimir Putin aliwaambia maafisa wa kiintelijensia jana Jumanne kwamba kumekuwa na idadi inayoongezeka ya matukio yanayohusu hujuma na ujasusi ndani ya Urusi. Ameitaka idara yake ya usalama kuchukua hatua zaidi