USA: Hapa ndio polisi wameua mmoja tu, hali iko hivi ya maandamano. Wangekuwa watatu au zaidi unadhani ingekuwaje?

USA: Hapa ndio polisi wameua mmoja tu, hali iko hivi ya maandamano. Wangekuwa watatu au zaidi unadhani ingekuwaje?

The Palm Tree

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
7,951
Reaction score
12,541
Hii ndiyo USA. Polisi kwa kutokuwa makini na kwa kukanyaga sheria zinazowaongoza kufanya kazi zao wakaua RAIA MMOJA TU asiye na hatia na asiye silaha kabisa huku wakiwa wameshamkata.

Hali iko hivi. Serikali nzima iko kwenye misukosuko. Inasemekana watu ilibidi waingie kwa nguvu hadi kwenye ofisi yao ya umma (White House) aanamoishi waliyepangisha kwa sasa, Donald Trump.

Kwa usalama wake, duru zinatonya kuwa ilibidi wamwondoe na kumkimbiza mahali pengine salama kwake.....

Najaribu kufikiri hali hii ingekuwa nchi za dunia ya tatu hususani hapa Tanzania ambako viongozi waliochaguliwa na wananchi wenyewe walishajipa hadhi wasiyostahili ya "U-mungu Mtu", mambo yangekuwaje?

Ni wazi, kumlinda mtu mmoja ingebidi waue mamia.

Hii ndiyo maana ya "PEOPLE'S POWER" ama kwa lugha ya kindendeule sema "NGUVU YA UMMA". Hii haijali bunduki wala mabomu ya machozi wala "kanuni za uchaguzi za mwaka 2020"

Likiwaka, limewaka. Lazima kieleweke.

Here is the video. Watch it for yourself.

 
... saa hizi polisi wangekuwa wameshaua wengine 100 katika kujaribu kuzima maandamano kabla jeshi halijaingia mtaani kuchapa risasi kila wanayemwona mbele yao. Hizo ndio shitholes!
 
Wameshawaua wengi sana. Labda sio mfuatiliaji tu. Hii ya sasa imekera zaidi sababu kauawa kwa mikono ya askari huku kamera zikishuhudia.

Labda umesahau usemi huu wa wahenga;

"......za mwizi ni arobaini....."

Utazoea kuiba pengine hata kuua mara ya 1,2,3.....39. Lakini 40 yako ipo tu usipoacha na kujirekebisha/kutubu....

Ndiyo wameua wengi kama hapa kwetu walivyokwisha ua wengi, lakini hii ndiyo 40 na hapa kwetu inakuja...

"Karma" haina longolongo.....
 
Labda umesahau usemi huu wa wahenga;

"......za mwizi ni arobaini....."

Utazoea kuiba pengine hata kuua mara ya 1,2,3.....39. Lakini 40 yako ipo tu usipoacha na kujirekebisha/kutubu....

Ndiyo wameua wengi kama hapa kwetu walivyokwisha ua wengi, lakini hii ndiyo 40 na hapa kwetu inakuja...

"Karma" haina longolongo.....
Sasa wewe unadhani silaha za police kazi yake nini? Kuwindia wanyama au?

Ukiwa mhalifu utauawa tu.
 
Sasa we unadhani silaha za police kazi yake nini? Kuwindia wanyama au?

Ukiwa mhalifu utauawa tu.

Aaah😳😳😳 kumbe ndiyo uelewa wako huu!!??

Wanaotoa "oda" ya "ua huyo" ndiyo hasa wahalifu na hizo silaha zingefaa ziwaue wao....

Bahati mbaya kwako ni kuwa, kwa "UJINGA" wako (siyo tusi pls, ila maana yake 'kutokuelewa kwako') unatetea wahalifu halisi pasipo kujua...

Matokeo yake ni hayo. Wasio na silaha wako mitaani. Wenye silaha wameweka mikono nyuma na silaha (bunduki) zao chini...

*Mwenye haki", Asiye mhalifu ndiyo huyo ameikimbia ikulu yake...!!

Bado tu hupati picha who is real criminal??

Pole yako bibie....
 
Sasa we unadhani silaha za police kazi yake nini? Kuwindia wanyama au?

Ukiwa mhalifu utauawa tu.
Wewe ni mpumbavu kama walivyo wengine tu,nyie ndio mawakala wa ibilisi duniani ,nani kakwambia adhabu ya muhalifu ni kifo? Sheria na mahakama za nini sasa,na nani kakwambia polisi ni hakimu nyie ndio mkiwa viongozi mnakuwa madikteta,pumbav.
 
Hii issue inachangiwa na pande mbili; upande wa kwanza lazima vyombo vya ulinzi na usalama vijue wajibu wao kwa watu wake, kulinda raia na mali zao; na upande wa pili; raia binafsi lazima wajue haki zao na wawe tayari kuzipigania.

Hapa kwetu sina shaka sana na kundi la pili la raia kutekeleza wajibu wao, hasa kwenye kudai haki zao ambazo kimsingi huminywa na vyombo vya ulinzi na usalama kwa lengo la kuilinda serikali.

Inahitajika reform ya hali ya juu kuwafanya polisi wetu watambue jukumu lao sio kuilinda serikali hata kama inawalipa mishahara, jukumu la polisi ni kuwalinda raia wake, tena bila kujali itikadi zao, watakapobadilika mitazamo yao ndipo taifa litasonga mbele.

Wakati mwingine serikali inawanyima raia haki yao makusudi kwa msaada wa polisi, na polisi wanatumika kufanya uhalifu kwa raia wa nchi hii bila wao kujua, kwasababu kama jambo fulani mf. maandamano ni haki ya raia kisheria, polisi wanapokataa kutoa kibali cha maandamano nao wanakuwa wameshiriki uhalifu kwa raia wake, haya mambo yanatakiwa yaishe.
 
Kwa nini unasema wameua mmoja? Polisi US walishaua weusi wengi! Ni tabia ya miaka yote na nadhani ungekuwa makini, ungeelewa kwamba sababu ya maandamano siyo huyo mmoja, ni maandamano kupinga mfumo bahati mbaya ni mfumo wa rangi. Hili siyo suala la sheria, siasa, vyama, n.k.
 
Siku watz wakiacha unafiki na ukondoo tutafika uko na ndipo titajua kuwa tulikuwa tumepumbazwa kiakili na CCM.
 
... saa hizi polisi wangekuwa wameshaua wengine 100 katika kujaribu kuzima maandamano kabla jeshi halijaingia mtaani kuchapa risasi kila wanayemwona mbele yao. Hizo ndio shitholes!
Muroto anawaona polisi wa huko wanakuna nazi tu
 
Sasa we unadhani silaha za police kazi yake nini? Kuwindia wanyama au?

Ukiwa mhalifu utauawa tu.
Kwa hiyo unaona sawa Serikali kununua silaha za kuua Raia wake na wala isinunue madawa ya Kuponya Raia wake?
 
Back
Top Bottom