Naona picha umezichanganya sana hadi kunakosekana mpangilio mzuri.
Kama sikosei kilichotokea hapo ni kuwa:
Ile Space plane ikiondoka Florida launching station, ikishapita kama sekunde tano tu, watu wanalijua hilo dude nje na ndani ndiyo huwa wanaanza kuliongoza yaani Houston. Ndiyo maana kumezuka msemo maarufu kuwa "Houston, we have problem".
Sasa hili dude likitoka huko MAJUU ya kikweli, huwa linarudi nyumbani kwako moja kwa moja yaani Houston. Hapo huwa wanaanza kazi ya kusafisha, kubadilisha vitofali vya chini ya tumbo lake, kuangalia kila chombo kama kiko kwenye good shape na kufanya matengenezo. Wakimaliza, basi huwa inakuja hiyo Jumbo Jet ya NASA yaani Boeng 747 na kubebeshwa hilo Dege baya (Space shuttle). Wanatake off pamoja na kutua Florida kwenye Station ya NASA. Wakilifikisha hapo, wanalipeleka kwenye jengo moja refu saaana. Hapo huwa wanakibeba na kukiunga kwenye matanki ya mafuta. Wakimaliza hapo laja likifaru moja (sijui hata niliige gari?) na wanaweka kila kitu juu yake na kubeleka kwenye launching Pad na kusubiri muda muafaka. Dakika kama tano kabla, ndiyo wanajaza MAFUTA kwenye tanki kubwa na kusubiri kulilipua. Wakilirusha tu, Houston wanaanza tena kulilinda dude lao na historia hujirudia.