Nikuwa kwenye boma la familia yangu huko Ununio nikajiuliza. Kwanini kuna uchafu wa mazingira wakati watu wana uwezo? Ukweli ni kwamba usafi ni utamaduni na sio uwezo au hata siasa.
Usafi inabidi uwe utaratibu. Hata kwenye familia yangu binafsi kwenye hilo hilo boma moja kuna familia moja kati yetu walikuwa wameweka shimo la taka kwenye kiwanja changu nikawaambia waache mara moja kufanya hivyo badala yake waanze kulipia wachukua uchafu. Nikagundua wachukuwa uchafu nao wanachukuwa na kwenda kutupa mitaroni ! Hivyo ni kuhamisha tatizo.
Serikali za mitaa pamoja na kuhimiza usafi na kuweka faini ni lazima waweke utaratibu mzuri wa mataka taka. Rwanda wamewezaje!?
Manispaa kwa wenzetu pesa ya taka inaongezwa kwenye pesa ya maji halafu kila wiki mmoja magari ya taka yanapita kuchukuwa matakataka hivyo unalipia kama hutaki au unataka . Hivyo nashauri gharama za taka ziwekwe kwenye maji lakini Serikali za mitaa zifanye kazi yake na kuwapa watu haki zao sio kuchukuwa pesa bila huduma