SoC01 Usafi ufanyike bila ubaguzi wa jinsia

SoC01 Usafi ufanyike bila ubaguzi wa jinsia

Stories of Change - 2021 Competition

Aryammy

New Member
Joined
Sep 15, 2021
Posts
1
Reaction score
0
Usafi ni kitendo cha kuondoa uchafu,vumbi na vitu visivyohitajika tena ilikuweka mazingira katika hali ya usafi na kujikinga na bacteria hatari na vijidudu .

Uchafu ni mkusanyiko wavitu mbalimbali visivyohitajika tena kwa matumizi kama vile mabaki ya chakula ,maji machafu , makaratasi .

Dhamira ya usafi imepotea tangu jamii inamuona mwanamke au msichana ndo anapendeza zaidi kufanya usafi na kuwa msafi muda wote, hali hii imepelekea watoto wakiume kuona kama jukumu la usafi ni la dada zao .

Lakini kumbe thamira kuu ya usafi si tu kueweka mazingira katika hali ya usafi bali pia kujikinga na magonjwa mbalimbali ya mlipuko na magonjwa mengine. Aidha masomo ya shuleni yanatufundisha bila kutilia mkazo katika swala la usafi hii inafanya jamii iwe na mtizamo tofauti juu ya swala la usafi.

Toka tupo watoto tumekuwa tukiambiw a tufanye usafi kuhofia kuitwa wachafu na wavivu ilikuwa uchague kuwa msafi au mchafu/mvivu

Wapo wanaochagua uvivu/uchafu akiamini akiitwa hivyo hakuna jambo litabadilika .

Lakini kumbe kufanya usafi hakukufanyi uonekane msafi tu bali pia kwakuweka mazingira , mwili na vituvinavyotuzunguka safi hutufanya kuwa na afya njema na maisha salama.

Hii dhana ikiwekwa kwa vizazi vyetu vinavyotufata tunaweza kupunguza idadi ya wachafu na wavivu kwakuwa kila mtu atakuwa na wajibu wa kuweka afya yake salama kwa kuwa msafi.

Jamii inatakiwa itufunze haya juu ya usafi
1 . Kuwa msafi ni jukumu la lazima kwa watoto wote .
Kila jinsia inajukumu la kuwa msafi kuoga ,kupiga mswaki kusafisha mazimgirana kadhalika

2. Waelekezwe na kusisitizwa kuwa usafi ni kwa afya yake.
Waswahilo wanasema mtoto umleavyo ndivyoakuavyo ,hili litakuwa jepesi kama litazingatiwa kipindi mtoto akiwa mdogo akipewa maarifa ya usafi katika afya yake

3. Elimu izidi kutolewa nyumbani na mashule kuhusu umuhimu wa usafi kwa afya .

Tusibaki kusoma usafi kama mada katika somo la biologia mbali itiliwe mkazo ili itupe maarifa mapana zaidi

4. Usafi ufanyike bila ubaguzi wa jinsia hii itajenga uwelewa zaidi.
Usafi usiwe tena wa mtoto wakike bali kwa watoto wote na kusisitiziwa kufanya hivyo kutamfanya kujua wajibu wake .

Tukiweza kuzingatia dhamira ya usafi tutatokomeza magonjwa sugu ya mlipuko kama malaria, UTI, minyooo, kipindupindu cha mara kwa mara. Kwasababu kila mtu atakuwa na jukumu la kulinda afya yake kwa kuweka mazingira safi na salama kwa afya.

Usafi ni afya😄

Muwe na siku njema.alamsiki
 
Upvote 0
Back
Top Bottom