Injinia,
Hayo ndio masharti Serikali iliopewa kwene haya ma-SEAP na madudu mengine, kwamba serikali isijishughulishe na utoaji huduma na badala yake kazi hiyo ifanywe na watu binafsi. Cha kusikitisha ni kwamba hakuna uboreshaji wowote wa maana ambao tunaeza kusema umepatikana na hizi sekta binafsi. Na kituko zaidi, kwenye kadhia kaa hizi anayefaidika ni mwenye kampuni. Utakuta yupo town anasukuma ndinga ya maana thanks to tenda ya halmashauri , ilhali hao wamama wafagizi(mind you, wengi wao ni wajane) wanalipwa pesa mbuzi ambayo huezi kuamini. The same stupidity in policy ndio unakutana na kadhia kaa ile ya akina Kingunge na kituo cha mabasi Ubungo. With this same spirit ndo unakuta mpaka ukarabati wa kawaida wa mabarabara ya vumbi huko mawilayani wanapewa hadi Wachina halafu eti tunakaa tunaulizana kwanini tu maskini? Are we for real?
Lakini kinyume chake, serikali inge-take charge ya kusimamia shughuli hizi kwanza ingetoa ajira kwa watu wengi zaidi kwa sababu kusingakuwa na sababu ya kulipa zaidi kwa mwenye kampuni binafsi. Pili ingeweza kuwa kusimamia utekelezaji na ku-link na shughuli nyingine kama maboresho ya sehemu za madampo et etc..