Julimycota
New Member
- May 4, 2020
- 3
- 2
Sera ya mazingira ya taifa ya mwaka 2021 imehusianisha Moja Kwa Moja Utawala Bora na Usimamizi wa mazingira. Katika Sura ya Kwanza, kipengele Cha pili, kifungu Cha tisa inasema kwamba, Utawala Bora ni nguzo muhimu Kabisa "central component" katika Usimamizi wa mazingira. Pia miongoni mwa malengo ya Sera hii ni kuhamasisha utawala Bora kwenye Usimamizi wa mazingira katika ngazi zote za uongozi.
Utekelezaji wa sera hii umechochea ushirikishwaji wa wananchi katika mipango ya Usimamizi mazingira, na pia kuajiriwa kwa maafisa mazingira katika ngazi ya wizara, mikoa na wilaya.
Sera hii pia imehimiza ushirikishwaji wa sekta binafsi, wadau wa maendeleo, mashirika ya Kidini na asasi za kiraia katika kusaidia Usimamizi wa mazingira. Shirika kama Nipe fagio limejikita katika kuratibu Usimamizi wa taka za plastiki. Makundi mbalimbali ya vijana na kina mama pia yamejiingiza katika biashara ya ukusanyaji na usafirishaji wa taka ngumu kutoka katika maeone yanapozalishwa na kupelekwa Dampo.
Sehemu ya pili ya Sheria ya mazingira ya mwaka 2004 inataka katika kila ngazi ya utawala kuwepo na afisa mazingira(na vigezo anavyopaswa kuwa navyo) ambaye majukumu yake pamoja na kamati ya Mipango miji ni kuhakikisha Sheria hii inatekelezwa kikamilifu.
Leo hii ni halmashauri ngapi, kata ngapi,vijiji vingapi, mitaa mingapi Ina Hawa wataalamu!? Au watendaji ndo wametwishwa mzigo huu ambao hawana taaluma nayo?
Serikali za mitaa Zina uwezo kiasi gani wa kusimamia ukusanyaji, uhifadhi, usafirishaji, utenganishaji, uokoaji rasilimali "resource recovery", na utupaji taka taka unaozingatia usalama na afya za wananchi wake!?
Je, kama wanataaluma hawapelekwi katika ngazi za chini za uongozi na Usimamizi, waliobaki wanaweza kutekeleza wajibu wao kama sehemu ya 9 ya sheria hii inavyowataka!?
Mtawala Bora anajua mahitaji ya anaowatawala, na anajihami kukabili janga kabla halijatokea. Mtawala Bora hasubiri mlipuko wa magonjwa Kisha aende kutibu waathirika.
Mtawala Bora atajali mazingira wanapoishi watu wake na atapambana kuyaboresha(kama mradi wa mitaro kule Kiwalani na maeneo ya Tabata) kulinda afya zao na haki Yao ya kikatiba ya Kuishi.
Sehemu ya 14 ya Sheria hii inawapa wanajamii haki ya kushiriki katika kutoka maamuzi yanayohusu masuala ya mazingira na mara kadhaa tumeshuhudia wizara husika ikiwaalika wadau kushiriki midahalo "Public hearing" juu ya mada mbalimbali Kwa mfano matumizi ya mifuko ya plastiki.
Basi ni wito wangu Kwa serikali, watu binafsi, wadau wa maendeleo, mashirika ya Kidini na asasi za kiraia kushiriki katika usimazi wa mazingira Kwa kufuata taratibu na miongozo ya nchi.
Pia jamii na viongozi wa ngazi za chini wajengewe uwezo katika kutambua na kuratibu shughuli zinazoweza kupunguza mzigo wa taka ngumu, maji taka na uharibifu mwingine unaotajwa na seya yetu ya mazingira.
Tuwajibike wote kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki, utupaji taka holela, ulipaji ada za kukusanya taka, kupunguza uzalishaji wa taka, kutumia nishati mbadala, na ubunifu wa teknolojia mpya zilizo rafiki katika kisafisha maeneo yetu.
Pia serikali isisite kuwatumia wataalamu wa mazingira waliowasomesha Kwa mikopo Yao, katika ngazi za chini ili kuchochea ufanisi na uwajibikaji katika Usimamizi mazingira kama sera yetu inavyotuhimiza.

Upvote
5