#COVID19 Usafiri kwenda Beijing, mji mkuu wa China, ulisitishwa ndani ya wigo wa hatua dhidi ya Virusi vya Corona

#COVID19 Usafiri kwenda Beijing, mji mkuu wa China, ulisitishwa ndani ya wigo wa hatua dhidi ya Virusi vya Corona

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Kulingana na taarifa ya South China Morning Post, ili kuzuia kuenea kwa virusi aina ya Delta vya Kovid-19 huko Beijing, baadhi ya ndege za kwenda jijini pamoja na huduma za treni na mabasi zilisimamishwa.

Zaidi ya watu 350 wameambukizwa virusi katika miji 27 baada ya aina mpya ya Kovid-19 inayoambukizwa kwa kasi zaidi kuripotiwa kwa mara ya kwanza katika mji wa Nanjing, mkoa wa Jiangsu mashariki mwa China.

Akizungumza kwenye mkutano wa Chama cha Kikomunisti katika mji mkuu, Katibu wa Chama Jai Qi alisema kuwa mji mkuu unapaswa kulindwa "kwa gharama yoyote", na hatua za haraka zaidi na kali kuamuliwa.

Wakati kesi 4 zimeripotiwa kutoka Beijing hadi kufikia sasa, viongozi wa jiji wamekubali kuongeza hatua za vizuizi za kuingia kwa watu wanaokwenda mji mkuu kutoka maeneo hatarishi, kama tahadhari dhidi ya kesi mpya ambazo zinaweza kutoka maeneo ya karibu.

Kama sehemu ya hatua hizo, kila mtu katika miji ambayo virusi aina ya Delta vya Kovid-19 viligunduliwa alikuwa amepigwa marufuku kuingia mji mkuu wa Beijing, na huduma za usafiri wa ndege, treni na mabasi ya mijini kutoka katika maeneo haya zilisimamishwa.

Ilionekana kwenye maeneo ya kuhifadhi nafasi kwamba tikiti za treni hazikuwepo kwa mikoa ya Nanjing na Zhangjiajie, ambapo virusi vilikuwa vikienea.

Wafanyikazi wa taasisi za serikali na biashara zinazomilikiwa na serikali walipigwa marufuku kusafiri kwenda miji iliyo na virusi, na taasisi zilikatazwa kusafiri kwenda katika mikoa hii.

Wakazi wa Beijing katika moja ya miji hii hawataweza kurudi jijini bila karantini ya siku 14 na matokeo yanayoonyesha hawana maambukizi.
 
Delta ni mbaya sana
Delta inaupiga mwingi bado Lambda ndio inakuja kumaliza mchezo
 
Hawa wachina Chanjo walichoma inakuwaje
 
China huwa namkubali kwenye kudhibiti huwa halembi ni amri na inatekelezwa mara moja sio huku Bongo mamlaka zina demka na porojo porojo za 666 .

China ni lockdown,chanjo na kupima kila mtu awe amepima, unfortunately ukikutwa mgonjwa treatment yako ni bora hata ufe wengi wapone.

Serikali inasema hivi eti wengine wanaopinga hadharani na kuhamasisha uasi wa umma na wanaachwa tuu
 
Back
Top Bottom