MIMI BABA YENU
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 305
- 728
Mnamo Desemba 14, 2019 Watanzania walipokea ndege ya nane iliyonunuliwa na serikali ya Dkt John Magufuli katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake uliotukuka.
Ununuzi wa ndege hizo ni miongoni mwa jitihada zinazofanywa na serikali kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).
Jambo hilo linaenda sambamba na ununuaji wa rada nne ambazo hutumiwa kuongozea ndege.
Kufuatia hatua hizo adhimu, mapato ya ATCL yameongezeka kutoka Sh. Bilioni 11.7 mwaka 2015/16 hadi Sh. Bilioni 45.5 mwaka 2018/19. Fedha hizo hutumika kuendesha shirika hilo, sambamba na kuchangia maendeleo ya taifa.
Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2019, jumla ya watu walioajiriwa na ATCL ilikua ni 521, wengi wao wakiwa ni watanzania.
Hakika maendeleo katika shirika hili yatasaidia kukuza sekta ya utalii, na kuongeza ajira hivyo kuwawezesha waajiriwa wa shirika hilo na Sekta ya utalii kuwa na uchumi wa Kati