A
Anonymous
Guest
Kumekuwa na kero ya muda mrefu sasa katika daladala za Mbweni jambo ambalo limekuwa usumbufu kwa abiria
Kwa mujibu wa LATRA route ya daladala za Mbweni ina Njia mbili
1. Kuna daladala zilizoandikwa Makumbusho au Simu 2000 - Mbweni zinapita Mbweni road (Masaiti na Malindi Jeshini)
2. Njia ya Pili ni ya daladala zilizoandikwa makumbusho au simu 2000 -Mbw/Mwisho.
Hizi daladala kwa mujibu wa LATRA zinapaswa kupita (via)Tanganyika road na Moga road, Lakini Daladala zote wakati zikitoka mjini (Makumbusho au Simu 2000) zimekuwa zikipita njia moja ya Masaiti kwenda Jeshini na kuwashusha abiria wa Teta na Mpiji eneo la Ubungo hivyo kulazimika kupanda pikipiki kwenda maeneo yao husika.
Wakati wa kurudi zote zinapita Mpiji na Teta (Moga road na Tanganyika road)
Hivyo abiria tunanyanyasika sana na hii kero nilishawahi kuwasilisha kwa mamlaka lakini utekelezaji wake umekuwa zero.
Kwa uchunguzi wangu nimebaini mambo mawili kwa madereva na makondakta
1. Wakati wa kwenda Mbweni wanapita Mbweni road bila kupita njia walizoandikiwa kwa sababu wanawahi kufika eneo husika ili wawahi kugeuza bila kuwajali abiria waliowabeba.
2. Wanapita njia ya Mpiji na Teta (Moga road na Tanganyika road) kwa sababu abiria ni wengi maeneo hayo bila kujua kuwa pia ni abiria wengi wanaoshuka maeneo hayo hivyo kujali maslahi yao binafsi kuliko kujali pia maslahi ya abiria wao.
Mwisho abiria tunalazimika kupanda pikipiki au kwenda kushuka Mbweni Msikitini na kusubiri gari jingine linalotosha mwisho ili kupanda tena na kulipa nauli nyingine, kitu ambacho ni kero kwetu kwa maana sehemu ambayo napasawa kulipa nauli ya gari moja tunalazimika kulipa nauli Mara mbili.