Usafiri wa kidigitali (taxify) watinga Mwanza

Mamayoyo12

Senior Member
Joined
May 30, 2018
Posts
182
Reaction score
41

Wananchi na madereva tax wa mkoa wa mwanza wamehimizwa kuchangamkia fursa mpya ya usafiri wa kidigital wa taxify. Taxify itaongeza ajira na kipato kwa madereva tax jijini mwanza na unafuu wa nauli kwa abiria watakaoita usafiri kupitia simu za mkononi popote waliopo

=======

WANANCHI na madereva 'tax 'wa mkoa wa Mwanza, wamehimizwa kuchangamkia fursa mpya ya usafiri wa kidijitali ( mtandao) ya Taxify .

Akizungumza katika uzinduzi wa huduma hiyo Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Mary Onesmo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo, John Mongella, alisema huduma hiyo itapunguza gharama na muda wa kusafiri.

"Taxify itaongeza ajira na kipato kwa madereva teksi jijini Mwanza na unafuu wa nauli kwa abiria watakaoita usafiri kupitia simu za mkononi popote walipo," alisema.

''Cha msingi ni kuikamata fursa hiyo na watambue kuwa huduma hiyo itanufaisha watu wengi wakiwamo wenye ulemavu na wazee waliokuwa wanataabika kutembea umbali mrefu kutafuta usafiri wa teksi,'' alisema

Kwa upande wake, Ofisa Uendeshaji Taxify Mwanza, Milumbilwa Kipimo aliwataka madereva teksi kujisajili na kwamba kampuni hiyo itatoa punguzo la asilimia 50 ya gharama ya usafiri kwa abiria kati ya Mei 28 na Juni 30, mwaka huu

"Gharama ya usafiri kwa kipindi hiki ni Sh 700 kuanza safari, Sh 460 kwa kilomita moja na Sh 70 kwa dakika moja," alifafanua

Ofisa Uendeshaji Taxify Tanzania, Remmy Eseka alisema jiji la Mwanza ni pili kufikiwa na kampuni hiyo nchini, likitanguliwa na Dar es Salaam ambako ilianza kutumika mwaka 2017 lakini Taxify inaunganisha watumiaji na watoa huduma ya usafiri ulimwenguni kote.

Mwenyekiti wa madereva teksi Mwanza, Beatus Mirambo alisema wameipokea Taxify lakini elimu ya huduma ya usafiri kidijitali inahitajika kwa wadau, ingawa kuna changamoto kwa baadhi ya madereva na abiria kutokuwa na simu zenye uwezo wa kuingia kwenye mtandao (smart).

Chanzo: Nipashe
 
eeee! hebu fafanua zaidi, nimeipenda hii habari
 
Ni vizuri mkijiimarisha Mwanza kabla Uber hawajatinga maana kwa Dar wamelishika soko haswa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…