Habari ya kazi Your Excellency,
Ni mimi tena ndugu yako katika kujenga taifa hili. Mimi Yusufu Sabura.
Moja kwa moja niende kwenye mada husika.
Kwa niaba ya wanaotumia mawasiliano ya Barabara ya kilwa road, ama kwa umaarufu route ya mabagala-kisemvule, ninayo hamu ya kufikisha ujumbe huu hapo mezani kwako.
Binafsi nadhani kama tutakusanya route zinazotia hasira wakati wa safari hapa jijini Dar Es Salaam ni pamoja na hii ya mbagala kisemvule. Route hii ina kero za namna mbili kama ifuatavyo ;
- Ajali za mara kwa mara kipande cha kuanzia pale kwa MO unateremka mtoni hadi kongowe, ajali hizi zinasababisha jam ya foleni kubwa sana ya hata masaa mawili. Kwa wanaotumia Barabara hii ni mashahidi kuwa ikipita siku bila lori kumwagika pale kwenye kilima basi tunashukuru Mungu.
Marudio ya hizi ajali wakati mwingine tunajiuliza au ni njama dhidi ya mbio za urais hapo Oktoba ? (kwa wageni kama mimi). Au kuna mchezo mchafu huwa unaendelea maeneo hayo na ajali hutumika kama mwamvuli kufanikisha a certain illegal mission?.
Mheshimwa Rais na dada yake na Paskali, Barabara ya kilwa road inakuchafua kuliko Lissu alivyomchafua mbowe, tafadhali zingatia hili, kwa maana kila tunapokuwa kwenye foleni wananchi huwa wanalalamika na kuuliza je ! ina maana Samia halioni hili?, kwa vile wewe hupandi daladala huwezi kulisikia lakini sisi mashabiki zako wa kisiasa hapa jamvini tunapanda daladala na tunayasikia, Your Excellency please take this issue to your considerations.
- Uhaba wa gari za usafiri kila ifikapo saa kumi na mbili jioni.
Your excellency, hili suala linatia kichefuchefu sana, kwa sababu hata kukiwa hakuna foleni kupata gari ya kisemvule usiku imekuwa kipengele kigumu sana, gari zote huhamia route ya mbande na chamazi huku wasafiri wa kisemvule wakisubiri miujiza ya Mungu itokee.
Inaweza kuchukua saa nzima kusubiri usafiri wa kisemvule ufike, na gari ikifika basi imejaa, nikuhakikishie Mheshimwa Rais kuna watu wanafika nyumbani karibia kwa nusu wiki saa sita usiku na kuamka saa kumi na moja asubuhi, sasa unajiuliza are we really in the 21st century? Wakati huohuo lawama zote ni kwa serikali na chama, there is no way tunaweza kukwepa lawama za wapiga kura wetu.
Your Excellency,
sisi wana kisemvule hatukupata mtume, tunakuomba umtume mtu aje kushughulikia masuala haya haraka iwezekanavyo ili hapo Oktoba tusitumie nguvu kubwa kubaki madarakani. Mimi naelewa Uchaguzi haujawahi kuwa rahisi.
Asante na kazi njema.
rajarajabu99@gmail.com