Usafiri wa Mwendokasi urekebishe mapungufu haya haraka

Usafiri wa Mwendokasi urekebishe mapungufu haya haraka

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Kuna siku moja nimetumia Usafiri wa Mwendokasi nikaanzia Gerezani, lengo langu nipande gari ya kwenda Mbezi halafu kutoka pale nitafute usafiri wa kwenda Mlonganzila Hospital.

Shida ilianzia hapo hapo nikaambiwa hakuna gari ya kwenda Mbezi, gari zote zinaishia Kimara halafu pale utaunganisha, nikashangaa. It was my first time, kabla ya hapo sikuwahi kupanda mabasi hayo, na kama wangejua kuna mnoko wa JF pale wangeficha baadhi ya ujinga wao.

Basi bhana abiria tukapangishwa foleni tukisubiri usafiri wa kimara, hadi dk 20 haijafika gari ya Kimara, nikashangaa kama huu ndio usafiri wa mwendokasi baadae gari ikaja, sisi tuliokuwa kwenye foleni ambao ndio tulipaswa kuingia kwanza tukawa wa mwisho, abiria wazoefu wanaingilia popote, wala hakuna utaratibu, hakuna tofauti na daladala za Mbagala au Gongo la mboto ambazo abiria wanaingilia madirishani ila hizi madirisha yalifungwa ndio tofauti yake.

Mabasi ya Mwendokasi hayajawahi kujaa, abiria wanapangwa utadhani kokoto za kujengea barabara, nilishangaa sana, ukiwa ndani ya basi hizo huwezi kuongea na simu ukaelewana na aliyekupigia, yana kelele mno utadhani mashine ya kusaga kokoto, injini inaunguruma moja kwa moja ndani ya basi.

Nilipokuwa kituoni gerezani niliona Mabasi mengi yamewekwa vibao vya maboksi chakavu ili kuonyesha yanakoelekea, nikashangaa sana, yaani tumefikia kuweka vibao vya maboksi chakavu kweli?

Nilipofika Kimara ndio jasho lilinitoka zaidi, nikasikia Matangazo mbalimbali yakielezea ruti zinazopatikana kwenye kituo hicho ambacho nadhani ndio kikubwa kuliko vyote vinavyotumika kwa sasa, lakini kama huna uzoefu huwezi kujua yanaposimama magari ya unakoelekea, vibao vya maboksi walivyoweka vimepauka wala havionekani!

Kwa kifupi Pale Kimara pana vurugu utadhani ni tamasha la kigodoro, hakuna mpangilio unaoeleweka wa ruti za mabasi yenyewe na nadhani wajanja wanaweza kupanda magari haya bure kabisa, hakuna ukaguzi wa maana wa tiketi, ukizubaa unaweza kupanda gari isiyokuhusu.

Kwa kufupisha niseme tu kwamba Mabasi ya Mwendokasi yanahitaji maboresho ya kiwango cha juu sana, kuanzia mabasi yenyewe, utaratibu, mipango, vibao vya matangazo , na utaratibu wa kupakia abiria, vinginevyo mradi huu hautafika hata 2025.
 
Wala usishangae KIONGOZI, ungeshangaa kama huo MRADI ungekuwa unafanya KAZI vizuri..

Hakuna mradi hata mmoja wa Serikali hii ya CCM huwa unafanikiwa..na hii ni kwa kuwa hawana HURUMA na wananchi..ndio!

Mradi wa ATCL chali
BRT- chali
TTCL chali
TRC - Ubadhirifu
Usafiri wa wakazi wa Kivukoni-Kigamboni- Chali
TAZARA - chalii..
Mradi wa Rada- digits ziliongezwa..
 
Mie sioni sababu ya kuendesha huu mradi kwa namna wanavyoe ndesha. Wao wangesimamia miundombinu. Halafu wangeruhusu mabasi binafsi lakini kwa idadi maalumu. Sio kukumbatia kampuni moja. Ushindani ungesaidia sana.
Wangeweka sera ya aina ya mabasi. Na kuwatoza watakaoweka mabasi kwenye njia hizo.
 
Back
Top Bottom