Usafiri wa umma watakiwa kubeba abiria kwa idadi ya viti 'Level Seat' ili kupambana na mlipuko wa Virusi Corona

kunguni wa ulaya

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
4,131
Reaction score
6,111
Katika mikakati ya kupambana na ugonjwa wa Corona (Covid-19) serikali kupitia Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani linasimamia kuhakikisha kila gari ya abiria inabeba abiria kulingana na idadi ya siti zilizopo.

Mfano leo huku Wilaya ya Kigamboni ikitokea daladala imejaza zaidi ya uwezo wake na wengine kusimama, wote waliosimama wanaamriwa kushuka na kusubiri usafiri mwingine.

Pia soma > Waziri Kamwelwe atangaza mkakati wa kupambana na ugonjwa wa Coronavirus kwenye vyombo vya usafiri

----
 
Afadhali kuchelewa kuliko kutoenda kabisa.
 
Sasa huoni kwamba wakisitisha kabisa athari kiuchumi ndio itakuwa kubwa zaidi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa route ya Ferry-Machinga complex ina daladala chini ya 10 siitakuwa balaa!
 
Kisemvule-posta ngoma level seat.
Tuombe maambukizi yasiongezeke.
Yakiongezeka ni mwendo wa kukaa ndani tu
 
Unataka look down sio bure ww

god is good
 
Hayo yote kupoteza mda serikali bado ijafanya kazi yake ya kuzuia kuenea kwa gonjwa hi la covid 19, distancing inayo hitajika ni mita moja kutoka mtu kwa mtu......

Sent using Jamii Forums mobile app
Naona jana baadhi ya misikiti imeshaanza kufungwa. Wakichukua hatua kuepusha mikusanyiko.


Huu msikiti upo Posta karibu na Hindu mandal hospital.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…