Usafirishaji wa mizigo toka South Africa

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,925
Naomba taarifa kuhusu usafirishaji wa mizigo kutoka South Africa kuja Tanzania. Je kuna usafiri wa meli au barabara unaoufahamu? Je kuna ameshawahi kusafirisha mizigo? Natanguliza shukrani.
 
Kama unafahamiana na mtu yuko shoprite muombe akudadisie hizo info kwa wale wanaopokea mizigo ya bidhaa zao toka huko(sa),kisha kama ni malori basi ujue ni ya watanzania ama waSA.km ni ya watz tafuta mawasiliano na dereva ndie anaweza kukupa majibu mazuri.
Kila la heri.
 
Njia rahisi mbili kwanza ni kwa meli,kama mzigo upo kule atafute cargo services ambazo ni nyingi sana na gharama yao ni nafuu sana ndani ya siku saba mzigo unakuwa bandarini na hii ni kwa mizigo mizito kama gari au vifaa vizito,njia nyingine ni ya ndege japo ni gharama kulingana na uzito wako lakini mtumaji akishatuma mzigo atapata namba (waybill) ambayo wewe utatumia kutolea mzigo wako uwanja wa ndege...kumbuka kutuma kwa meli ni gharama ndogo maana wanaangalia size ya mzigo wako (CBM)na utumaji wa ndege ni gharama maana unaangalia uzito...kutakuwa na njia ya magari lakini hii sina uhakika nayo..zaidi ni kwamba tuambia huo mzigo upo wapi hasa kama pretolia au j'sburg nk...kuna makampuni haya giga simu watakusaidia SKY AIR Tel +27110575351 au jingine +27113901159 linaitwa KF FORWARDERS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…