Usaha kwenye mapafu

Usaha kwenye mapafu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
empyema.bmp
thorencetisis.bmp


  • Ni muhimu mgonjwa kwenda hospitali kufanyiwa uchunguzi

Kitaalamu hufahamika kama empyema thoracis. Ni tatizo la kujaa usaha katika chumba kinachotunza mapafu ndani ya kifua (pleural cavity). Tatizo hili ni kubwa na lisipo tibiwa haraka, huleta madhara makubwa

ikiwa pamoja na kupoteza maisha. Hata hivyo, kupatikana kwa dawa za kuua vijidudu (antibiotics) kumesaidia kupunguza vifo na madhara mengine makubwa.

Tatizo hili husababishwa na magonjwa kadhaa ikiwa pamoja na homa ya mapafu (nyumonia- Pneumonia), jipu la mapafu au fangasi wa mapafu, Kifua Kikuu-TB, kuumia kifuani mfano kupata ajali au kuchomwa na kitu kikali, maambukizi ini kwa juu.

Mgonjwa huwa na dalili za homa kali, mwili kuchoka, kupoteza uzito, kukosa hamu ya kula, maumivu kifuani au mapafu, kifua kupindia upande ulioathirika, kupumua kwa shida, kukohoa na kutoa makohozi

hutokea kama mgonjwa ana TB na Nyingine ni njia za hewa kuunganika na chumba cha mapafu (bronchiopleural fistula) na jipu kifuani ambalo huweza kutokea kutokana na usaha uliondani kujipenyeza katikati ya mbavu. Jipu hilo huweza kupasuka, hivyo usaha mwingi kuchuruzika nje.

Ni muhimu mgonjwa kwenda hospitali kufanyiwa uchunguzi. Vipimo ambavyo huweza kufanyika na kubaini tatizo ni picha ya kifua (X-ray), kutoboa kifua na kuuvuta usaha kwa sindano, kisha kuupeleka maabara kwa uchunguzi, altrasound ya kifua ambayo husaidia kubaini wingi wa usaha au kama usaha upo katika vijumba

vidogodogo (septated), CT scan huweza kusaidia iwapo tatizo limekaa zaidi ya siku 3, kwani huweza kuathiri mapafu na kifua vibaya zaidi, hivyo humsaidia daktari katika uamuzi na kutoa matibabu sahihi.

Matibabu kwa tatizo hili ni kupitisha mrija kifuani kutoa usaha kwa chombo maalumu, mgonjwa pia hupewa dawa kali za kuua vijidudu, kama ana kifua kikuu basi dawa hutolewa pia. Kuzuia tatizo lisijiruide, dawa au

poda maalumu huingizwa katika chumba hicho cha mapafu baada ya usaha wote kuwa umetoka
(pleurodesis). Ikiwa mrija umeshindwa kutoa usaha basi uhitajika upasuaji wa kutoa sehemu ya mbavu moja

kisha kupisha mrija mkubwa zaidi kutoa usaha. Iwapo mgonjwa amekaa na tatizo hili kwa muda na mapafu yameathirika kwa kiwango kikubwa, upasuaji mkubwa hufanyika kukwangua uchafu wote, kuharibu vijumba na kutoa usaha kisha kusaidia mapafu kurudi walau katika hali ya kawaida.
Usaha kwenye mapafu - Makala - mwananchi.co.tz



 
Back
Top Bottom