Usaili wa ajira za ualimu hauko fair

Usaili wa ajira za ualimu hauko fair

Mkurya mweupe

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2023
Posts
239
Reaction score
817
Nimeshangaa kuona jamaa yangu mmoja leo ambae huwa ni dereva bodaboda karibia mwaka wa tisa sasa akisema ametoka kufanya interview ya ualimu, Kwanza nimeshangaa maana sikuwahi kujua kama ni mhitimu wa degree ya ualimu mwaka 2015 kutokana na kumuona yupo serious na kazi hiyo

Kinachonishangaza ni kwa jinsi gani mtu aliyepiga kazi ya uboda kwa miaka 9 ataenda kushindana na mhitimu wa ualimu wa mwaka 2024 au ataweza vipi kushindana na mhitimu wa ualimu ambaye kwa sasa anafundisha private school ?

Imebidi niwaze Jakaya Kikwete alitumia njia gani kuweza kuwa anawaajiri wahitimu wote kwa kigezo Cha mwaka, kabla mwendazake hajaharibu huo mfumo kwa kisingizio anatumbua watumishi hewa
 
Serikali haina namna ya kukwepa lawama ata wakifanya unavyoshauri. Binafsi naona bora wameacha huo mtindo wazamani maana wahitimu hawakuwa serious kujiajiri wakisubiri siku flan mkeka utatiki.

Sasahivi si wahitimu wapya wala wazamani watatupa lawama zao kwa serikali, bali watakaoshindwa usaili. Hao naona wajilaumu wenyewe.
 
Nimeshangaa kuona jamaa yangu mmoja leo ambae huwa ni dereva bodaboda karibia mwaka wa tisa sasa akisema ametoka kufanya interview ya ualimu ,Kwanza nimeshangaa maana sikuwahi kujua kama ni mhitimu wa degree ya ualimu mwaka 2015 kutokana na kumuona yupo serious na kazi hyo ......Kinachonishangaza ni kwa jinsi gani mtu aliyepiga kazi ya uboda kwa miaka 9 ataenda kushindana na mhitimu wa ualimu wa mwaka 2024 ....au ataweza vipi kushindana na mhitimu wa ualimu ambaye kwa sasa anafundisha private school ? .imebidi niwaze Jakaya Kikwete alitumia njia gani kuweza kuwa anawaajiri wahitimu wote kwa kigezo Cha mwaka ,kabla mwendazake hajaharibu huo mfumo ,kwa kisingizio anatumbua watumishi hewa
Wakati wa JK sera ya elimu Kwa wote ilikuwa ktk utekelezaji wake, shule za sekondari za kata zilioteshwa kila Kona hivyo uhitaji wa waalimu ukawa mkubwa, so jakaya hakuwa na muujiza wowote kama mnavyojiaminisha
 
Poleni sn walimu mateso hayo walikuwa wamezoea wahasibu,maofisa biashara Hila madokta ilikuwa kitonga TU hila supply imekua kubwa kuliko demand Haina jinsi lazima interview ifanyike
 
Serikali haina namna ya kukwepa lawama ata wakifanya unavyoshauri. Binafsi naona bora wameacha huo mtindo wazamani maana wahitimu hawakuwa serious kujiajiri wakisubiri siku flan mkeka utatiki.

Sasahivi si wahitimu wapya wala wazamani watatupa lawama zao kwa serikali, bali watakaoshindwa usaili. Hao naona wajilaumu wenyewe.
Ni kweli mfumo wa Tamisemi hawakuwahi kiajiri stashahada ya uzamili katika Elimu yaani PGDE so mwaka huu iliporejeshwa utumishi hatimaye wameguswa. Fikiri Kila mwaka Tamisemi walipotoa walionesha wanaostahili kuomba lakini Hawa hawakuchagiliwa tangu wakati wa Awamu iliyopita ya serikali. Hii iliumiza na kukatisha tamaa wale waliosoma hiyo ngazi Kwa Mapenzi Yao ktk Elimu na huenda Wana mipango wangesoma masters lakini matumaini Yao yalikufa Kwa hiyo miaka kadha.

So Kwa Hilo tuu namwombea Sana Katibu huyo Dr. Kiliba Kwa mwanga na kuondoa hiyo Bias ya wazi Kabisa.
 
Ajira za ualimu za JK ziliidondosha sana sekta ya elimu,waalimu walizembea matokeo yake likaibuka kundi la kuandika xaxa badala ya sasa au rara,nimekura.

Pongezi kwa JK kwa kuajiri ila kiwango kilishuka balaa
 
Tanzania inabid tuachane na summative assessment turud kwenye formative assessment ,ndo kipimo bora cha uelewa kwa ngazi zote
 
Kwa hiyo unataka dereva boda akafundishe watoto wako??
 
Back
Top Bottom