Usajili wa luku mpya

Usajili wa luku mpya

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
8,273
Reaction score
13,567
Habari za leo Watanzania?

Nilifungiwa mita ya umeme LUKU mpya takribani mwezi mmoja sasa.

Umeme uliwekwa units chache sana na tangu tarehe 05 Aprili 2024 nawasiliana na TANESCO makao makuu kuhusu suala hili na mara zote husema idara husika inalifanyia kazi suala langu.

Naomba kuuliza kwenu ni jambo la kawaida kukaa mwezi mzima bila mita ya umeme kusajiliwa na kuwezesha kununua token kupitia mitandao ya simu?

Binafsi nimechoka kukaa giza maana umeme haununuliki kwa kuwa mita yangu haijasajiliwa.
Watu wa TANESCO wamekuwa ni watu wa ajabu na maneno mengi yasiyo na maana yeyote.
 
Umeme Unaokuja Na Meter Ukiisha Ule Wa Kwanza Lazima Uende Ofisini Kwao Ili Waruhusu Meter Yako Kununua Umeme Kwa Mitandao Yote Na Banks
 
Sio lazma uende ofisini, piga ile namba yao, (japo utasubiri sana), then ongea na mhudumu mueleze suala.lako.
Atakuuliza mita namba, then atakutajia manamba kibao, utayarekodi pembeni then utaenda kufungua mita yako kwa kuingiza namba hzo.

Most times it takes at least 5 working days kuanzia wanapofunga mita mpya hadi kusajiliwa.
 
Kuna namba ambazo unatakiwa uingize kabla ya kuanza kununua umeme mara tu ule uliowekewa kuisha. Wanababaisha mithili ya kutoa kitu kidogo ili upewe hizo namba.
 
Nimeshawapigia huduma kwa wateja ya TANESCO zaidi ya mara 3 tangu tarehe 5 Aprili 2024 lakini hakuna solutions waliyofanya. Nchi imejaa watu wa ajabu sana kwenye ofisi za umma.
 
Nimeshawapigia huduma kwa wateja ya TANESCO zaidi ya mara 3 tangu tarehe 5 Aprili 2024 lakini hakuna solutions waliyofanya.
Nchi imejaa watu wa ajabu sana kwenye ofisi za umma.
Wana Uzi wao humu ndani watafute Huwa wako active kiasi.
 
Back
Top Bottom