BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Usajili wa magari kufanyika mara mbili kwa mwaka
Halima Mlacha
Daily News; Sunday,October 05, 2008 @20:04
KAMANDA wa Kikosi cha Usalama Barabarani, James Kombe, amesema katika kutatua tatizo la msongamano wa magari barabarani, usajili wa magari makubwa sasa utafanyika mara mbili kwa mwaka.
Pia amesema wanaandaa utaratibu wa kupiga marufuku kuingizwa kwa magari yote yenye umri wa miaka mitano nchini.
Akizungumza mwishoni mwa wiki katika mkutano wa waandishi wa habari Dar es Salaam, Kamanda Kombe alisema imebainika kuwa moja ya sababu kubwa inayosababisha msongamano wa magari barabarani ni kuwapo kwa magari mengi mabovu.
"Tunafahamu kuwa msongamano wa magari ni kero kubwa hasa katika majiji kama Dar es Salaam, ndio maana safari hii tumepanga registration ya magari makubwa itafanyika mara mbili kwa mwaka na itafanyika kwa kompyuta kama gari ni bovu litafutiwa leseni," alisema Kombe.
Alisema pamoja na magari hayo makubwa pia magari madogo nayo yatafanyiwa usajili na kukaguliwa mara tatu kwa mwaka na iwapo litakuwa na umri wa miaka mitano halitaruhusiwa.