Kwani hatuna chombo maalumu (NGO or otherwise) cha kupigania HAKI za wananchi? Maana serikali ya CCM imeacha kabisa kujali maisha yetu.
Chombo kama kipo basi kiende mahakamani kipate restraining order dhidi ya Kombe na hao waliomtuma. Maana katumwa huyo, sio hivi hivi.
Hii njia ya kupigania haki kupitia mahakama inafanya kazi wakati mwingine. Nakumbuka kuna kipindi serikali ilitoa amri mabasi ya Dar Express yasimamishe huduma zake (baada ya ajali mbili). Kwa vile mkuu wa hayo mabasi si mtu wa mzaha, alikwenda mahakamani na akaweza kulazimisha serikali isiyasimamishe mabasi yake.
Hawa wabaya wetu wananunua magari kwa kutumia fedha za umma, na wanabadilishiwa mengine baada ya miaka michache tu. Sasa wanadhani hata sisi tunaotegemea fedha za jasho letu wenyewe tunaweza kufanya hivyo?
Ieleweke hivi: Sehemu kubwa ya sisi Watanzania, hata wale ambao tumefuta ujinga, haijawahi kuendesha gari lenye umri huo mnaotaka wa chini ya miaka 5. Si kwamba hatupendi, ni hatuwezi. Sasa na hiki kidogo tulichonacho mnataka kutunyima?
Ni rahisi kwa wale waliovimbisha matumbo kwa kutafuna fedha za umma kufungua vinywa vyao (in between eating and drinking), na kusema SASA TUENDESHE MAGARI YENYE CHINI YA MIAKA 5 TU. Kilichobaki ni sisi kupigania haki zetu mahakamani. Au tuendelee na kawaida ya "kuwaomba watuonee huruma"?