Usajili wa namba za simu, piga *106# ok.

Ulimbo

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2009
Posts
3,768
Reaction score
4,038
:A S-rose:Wana JF,Nilisajili namba yasimu mwaka jana, nilikuwa naakikisha kama namba yangu ya simu - Vadacom imesajiliwa. Nilipopiga *106#, nilishtuka kupata jibu linaniambia kuwa sijasajiliwa.
Nikajaribu kuhulizia wenzangu kama wawili, ni wao pia wlipata ujumbe huohuo japo pia nao walisha sajili. Je hivi ni kweli nambazetu hazijasajiliwa wakati form za kujisajili tunazo?
Sijaangalia mitandao mingine kama ili tatizo lipo kwao.

JAMANI SIKU ZIMEISHI, CHEKINI NAMBA ZENU KAMA ZIMESAJILIWA.:A S-rose:
 
Mimi tiGo nao jibu ni hilo hilo hujasajiliwa wakati nilisajili tangu mwaka jana....huu si ubabaishaji jamani ?
 
hi ulimbo naomba nijulishe tigo kujua km nimesajiliwa nifanyeje maan napiga *106# cpati jibu
 
Hata mimi hivyo hivyo tigo nilisajili toka mwaka jana lakini inaniambia sijasajili,

Kwa tigo tuma ujumbe mtupu kwenda 106 watakuletea jibu
 
jaribuni kufuatilia.all my numbers naambiwa zimesajiliwa kikamilifu.tena wananiit dear....hahahahaaa
 
hapana bana mimi nimejaribu kufuatilia sana baadhi zimeniambia nimeshasajiliwa na nyingine zimeleta jibu la bado
 
Hasa wateja wa Vodacom ndio tumeathirika zaidi. Voda anza usajili on line
 
poleni ambao mlijisajili lakini leo bahati mbaya inaonekana hamjasajiliwa, tatizo ni agents waliowasajili, hapa kwetu walipita agents wa tigo na voda ofisini wakasajili wafanyakazi, lakini kuna agent mmoja sijui imekuwaje maana wote aliotusajili, fomu tunazo lakini uki-check unaambiwa hujasajiliwa, hatuelewi kilitokea nini, lakini hakuna jinsi ni kujisajili tena tu.
 
Duh mie nimesajiliwa kwa jina la mtu mwingine mwanamme loh
 
usumbufu,nahisi taarifa za mwaka jana zilifutika katika mtambo wao,zimeaza kuingia za mwaka huu tu he he he he

kituko kingine,leo asubui nimepiga *106# tigo nikaambiwa namba imesajiliwa ,mchana huu napiga tena ivo naambiwa "namba ulizoweka ni batili.huduma hii haijafanikiwa kwa sasa"
laaa watupe maelezo ya kina,ngoja nijaribu ku-sms 106
 
Huu ni usumbufu mkubwa. Niposajili line yangu, nilisajili pia m-pesa, lakusikitisha ni kwamba hata m-pesa sijasajiliwa. Nimeenda ofisi za vodacom, wakaniambia nilisha sajiliwa ndo maana ninaform, nikawasisitizia kuwa pamoja na kuwa na fomu, bado sijasajiliwa. Wakachukua simu yangu, wakabonyezabonyeza, wakaniambia hatawao hawajui kwa nini wanapata huo ujumbe kuwa sijasajiliwa.
 
Hii imemkuta hata wife wangu.....hatari kweli!

Hahahaha!!!!Mkuu inawezekana FL ni mkeo, siunajua tena JF na majina ya uoga, nenda naye chemba, utashangaa...nakujiuliza duh kumbe na wife ni member humu....lol
 
JAMANI SIKU ZIMEISHI, CHEKINI NAMBA ZENU KAMA ZIMESAJILIWA.:A S-rose:[/QUOTE]

kituko kingine::tsk:
1.baada ya kutuma sma 106 tigo nikapata jibu "namba yako imesajiliwa tayari",
2.muda huo-huo tu naambiwa "namba yako bado haijasajiliwa..kama ulisajili zamani tuma jina lako kamili na namba ya fomu kwenda 106" ......zamani???ndio nini???

WTF?????????????????????????this is absolutely bullshit nina hasira sana hapa,ivi wanafikiri hatuna shughul za maana sisi?

3.hivi hii huduma ni bure????(ngoja nicheki na salio)
 
JAMANI SIKU ZIMEISHI, CHEKINI NAMBA ZENU KAMA ZIMESAJILIWA.:A S-rose:

kituko kingine::tsk:
1.baada ya kutuma sma 106 tigo nikapata jibu "namba yako imesajiliwa tayari",
2.muda huo-huo tu naambiwa "namba yako bado haijasajiliwa..kama ulisajili zamani tuma jina lako kamili na namba ya fomu kwenda 106" ......zamani???ndio nini???

WTF?????????????????????????this is absolutely bullshit nina hasira sana hapa,ivi wanafikiri hatuna shughul za maana sisi?

3.hivi hii huduma ni bure????(ngoja nicheki na salio)[/QUOTE]


Mweeeeeeeeeeeeeeee. Kama hali ndivyo ilivyo, basi ifikapo huo mwisho tarehe 30.6.2010, watu wengi sana watajikuta wamefungiwa simu zao. Sijuhi ni nani atakaye wajibika ikiwa watu wamesajili na fomu wanazo, lakini usajili wao hautambuliki.:mmph:
 
tiGO wamezidiwa na kazi. yaani wanataka tena sie tuliosajili kitambo tutume tena maelezo yetu. hapo watasubiri sana na wala wasijaribu kufunga line yangu
 
Mweeeeeeeeeeeeeeee. Kama hali ndivyo ilivyo, basi ifikapo huo mwisho tarehe 30.6.2010, watu wengi sana watajikuta wamefungiwa simu zao. Sijuhi ni nani atakaye wajibika ikiwa watu wamesajili na fomu wanazo, lakini usajili wao hautambuliki.:mmph:[/QUOTE]

zitafungwa nyingi sana tu bila sababu za msingi(uvivu wao wa tigo) bora nijiandae kisheria zaidi!!tutafikishana mbali!!
 
Wakuu, nina wazo. Kwa muda mrefu haya makampuni ya simu za mikononi yametutafuna sana. Hebu safari na sisi tujaribu kuwatafuna. Ninashauri kila mwanaJF atoe nakala ya fomu aliyojiandikisha na tarehe moja ikifika tu na ukafungiwa simu yako wakati uliandikisha, tujikusanye na kudai fidia kutokana na makampuni hayo 'kutukosesha mamilioni tuliyotegemea kupata kutokana na simu zetu kuwa hewani....' or something like that, kama wanasheria wetu humu ndani wartakavyoshauri. wametula sana hawa jamaa sasa na sisi tuwale...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…