May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Ni kama vile imekuwa ni vigumu kukabiliana na changamoto ambazo Wenzetu huko nje hawana shida nazo, na kwa kuwa wameshakuja na matumizi ya taa za kuongozea Magari wakaishia hapo nasi tumebaki hapo hapo ili hali sisi tuna shida zaidi ya hiyo.
Huwa najiuliza hivi vyuo vyetu kama NIT wana nafasi gani kutafuta suluhu ya baadhi ya matatizo ya nchi?
Si wapewe assignment kama hizo waumize vichwa maana ndio field zao?
MAONI YANGU:- Kama inawezekana mita kadhaa kufika kwenye taa kutenganishwe kwa kuweka borders ambapo Bodaboda na Bajaji zikae kwenye lane yao kushoto ambako kutakuwa na kigingi mbele kitakachozuia Pikipiki na Bajaji kupita, kigingi ambacho kitakuwa kinafanya kazi sambamba na taa zile, ikiwaka nyekundu kinainuka, na sehemu ile ya kulia ambako Magari yanatumia kubuniwe namna ya kuweka vigingi vitakavyomfanya Bajaji au Boda asichague kwenda, kwa kuwa tairi la Bajaji au Boda si sawa na yale ya Gari hivyo nadhani haitokosekana namna ya kufanya Boda ashindwe kutumia kipande kile cha mita 50 au 100 kufikia kwenye taa.
Nakumbuka iliwahi kuongelea suala la camera, sidhani kama tutafanikiwa maana tuna changamoto ya rasilimali Watu, hapa ni machinery tu ndio itatuondoa kwenye hili janga.