SoC04 Usalama katika ujenzi wa miradi ya Sekta ya Uchukuzi

SoC04 Usalama katika ujenzi wa miradi ya Sekta ya Uchukuzi

Tanzania Tuitakayo competition threads

PAULMATOLI

Member
Joined
May 28, 2024
Posts
11
Reaction score
14
USALAMA KATIKA UJENZI WA MIRADI YA SEKTA YA UCHUKUZI
Sekta hii inausisha ujenzi wa miundombinu kama barabara, reli, madaraja, kingo za barabara, mitaro, kalavati na barabara ndogo ndogo za vijijini, serikali kwa namna ya pekee sana imejitahidi sana kuendelea kupambana na sekta hii kwa kujenga barabara nyingi za lami, reli kwa kiwango cha standard guage, madaraja hasa sehemu korofi na sehemu zinazounganisha maeneo muhimu kama vile daraja la busisi.

CHANGAMOTO:- Wizi mkubwa unaofanya na WATANZANIA ambao serikali na wadau mbalinbali wanalenga kuwakwamua kiuchumi na ndio watumiaji wakubwa wa miundombinu inayotengenezwa na serikali, na Uzembe mkubwa unaofanywa na wasimamizi wa serikali wanapokuwa wanakagua miradi hii wanakosa UZALENDO na WELEDI katika utekelezaji wa majukumu yao na kushindwa kutetea maslahi ya taifa kwa lengo la kuipata Tanzania tuitakayo.

Serikali isipofanya mambo yafuatayo basi kila mwaka itakuwa na kazi yakuendelea kufahya ukarabati na ukarafati katika miradi iliyokamilika. Mfano barabara iliyojengwa na mkoloni hadi sasa ni bora kuliko barabara iliyojengwa miaka 5 iliyopita ikisimamia na serikali kupitia wataalamu wake pamoja na wafanyakazi wengi wakiwa ni Watanzania.

MAMBO MUHIMU NAYOPENDA KUSHAURI KWAAJILI YA KUHAKIKISHA MIRADI HII INAFANIKIWA KWA LENGO AMBALO NI KUBORESHA MIUNDOMBINU AMBAO ITAKUZA UCHUMI WETU KWA KASI ZAIDI.

1. Kutoa elimu kwa watanzania badala ya kuiba vifaa vya ujenzi kama saruji, nondo, mafuta ya kuendeshea mashine basi wao ndio wawe walinzi wakuu na kuhakikisha miradi yote inajengwa kwa kiwango kilichokusudiwa ili miradi yetu idumu. Hapa ndio penye changamoto kubwa sana maana tunaiba mali zetu wenyewe tukijua tunamwibia mkandarasi ambae ni mchina au mturuki wakati yeye sio mtumiaji wa hiyo miundombinu na zaidi mbeye yetu tuna wasimamizi vipofu ambao bado watapokea mradi huo ambao sisi walengwa tumeiba vifaa na kuufanya ujengwe chini ya kiwango.

2. Kuweka sheria kali kwa wanao hujumi miradi hii, sheria ilenge kumdhibiti kibarua hadi msimamizi mkuu wa serikali na kampuni iliyochukua mradi. Na watakao kamatwa kwa kuhujumi miradi hii wachukulie hatua na taarifa zitolewe ili iwe kama onyo kwa wale wahujumu wengine. Hapa vibarua wanaiba sana saruji na vifaa vingine.

3. Wahandisi wanaotoka serikalini pia wachukuliwe hatua pale ambapo miradi ile inathibitika imefanywa chini ya kiwango na sio kuleana leana mkosaji kubadilishiwa majukumu. Hii itasaidia sana kuwa fundisho kwa wengine.

Naamini miradi hii ikifanyika kikamilifu basi malengo ya serikali na watu wake yatafikiwa kwa wakati na badala ya serikali kurudi kwenyw ukarabati basi itaendelea kukakilisha maeneo mengine ambayo yanauhitaji wa kupata miundombinu bora.

Tanzania tuitakayo inahitaji UZALENDO NA WELEDI.
 
Upvote 2
.Kuweka sheria kali kwa wanao hujumi miradi hii, sheria ilenge kumdhibiti kibarua hadi msimamizi mkuu wa serikali na kampuni iliyochukua mradi. Na watakao kamatwa kwa kuhujumi miradi hii wachukulie hatua na taarifa zitolewe ili iwe kama onyo kwa wale wahujumu wengine. Hapa vibarua wanaiba sana saruji na vifaa vingine.
Ni masikitiko, kwa kweli sheria ifuate mkondo wake.

Tanzania tuitakayo inahitaji UZALENDO NA WELEDI
Tunefanya uzalendo kuwawekea mikataba hao wazabuni toka nje yenye sheria ya kwamba ni lazima waajiri wazawa katika vibarua na walinzi.

Sasa kama hii inasuasua tunaweza kuamua kuwa. Katika kuajiri vibarua ibaki hivyohivyo lakini kwenye ulinzi tuboreshe kiasi: Tuwaruhusu hao wazabuni wa nje kuwa na jeshi dogo lenye vifaa na weledi katika ulinzi kushirikiana na walinzi wa ndani. Mfano kajeshi ka wachina/waturuki 12 wenye drones, camera na bunduki za umeme ili kusaidizana kiulinzi.

Ni lazima tuangalie haki kutendeka maana mwisho wa siku vitu vikipotea hasara tunapata sisi wananchi na mzabuni mkandarasi.
 
Back
Top Bottom