Usalama: RC Makalla awapa miezi 3 bodaboda kujipanga vizuri na kusajili vituo vya kupakia abiria

Usalama: RC Makalla awapa miezi 3 bodaboda kujipanga vizuri na kusajili vituo vya kupakia abiria

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla amewapa miezi mitatu chama cha bodaboda kuhakikisha wanajipanga na kusajili vituo vyao.

Naye mwenyekiti wa bodaboda amesema wameitikia mwito wa Makalla kwa moyo mkunjufu na wanawasiliana na Injinia wa Tarura ili zoezi lianze mara moja.

Lengo ni kuimarisha usalama mkoani Dar es Salaam.

Chanzo: ITV habari
 
Nakubaliana na Hili wazo zuri mno ila kinachotakiwa bodaboda vituo vyao waende kwa foleni Nani anaanza kupakia na Nani anafuata

Abiria waelezwe wazi wachukue bodaboda kituo Cha bodaboda kilichosajiliwa wasisimamishe bodaboda za njiani nyingi huwa za majambazi hasa usiku zinakuwa na namba bandia.

Elimu itolewe kwa abiria kuwa usichukue bodaboda nje ya kituo kilichosajiliwa.

Tarura waweke tangazo tv na Radio kuwa usichukue bodaboda nje ya kituo kilichosajiliwa
 
.... ndivyo sheria ya usalama barabarani na ile ya usafirishaji abiria inavyotaka? Ukipakia abiria nyuma kwenye pickup trafiki watakukamata kwa sababu sheria hairuhusu! Ukiendesha gari bila kufunga mkanda trafiki watakukamata kwa sababu sheria inakataza kuendesha bila mkanda!

Ni kipi kinahatarisha usalama zaidi? Bodaboda au bajaji ambazo hakuna cha mkanda; tena bodi ni mwili wako! Ifik mahali sheria nyingi za usalama barabarani na zile za usafirishaji wa abiria ziwe reviewed badala ya kupeleka mambo kisiasa! Hiyo ni siasa badala ya professionalism!
 
Hili wazo kuna mtu namjua alikuja nalo kuhusu boda boda wote dsm kote kuwepo na vituo.

Kuanzia kuwasajili, kuvaa uniform, kila boda anakuwa na namba maalum na wanawekwa wote kwenye data base.

Sema kuna mambo fulanifulani yalikwamisha

Siasa iliingia..ngj tuishie hapo

Ova
 
Hapo kwenye kusajili na kuwa na kituo basi hao tarula waweke vyoo vya kulipia Ili hao bodaboda watumie na waweke bati juu wakae chini ya bati siyo kukaa chini ya miti au hovyo hovyo kitu kinachofanya ajira zao kuwa za watu wengi wahuni.
 
.... ndivyo sheria ya usalama barabarani na ile ya usafirishaji abiria inavyotaka? Ukipakia abiria nyuma kwenye pickup trafiki watakukamata kwa sababu sheria hairuhusu! Ukiendesha gari bila kufunga mkanda trafiki watakukamata kwa sababu sheria inakataza kuendesha bila mkanda...
Basi wapewe leseni za kusafirisha mizigo.
 
Hapo kwenye kusajili na kuwa na kituo basi hao tarula waweke vyoo vya kulipia Ili hao bodaboda watumie na waweke bati juu wakae chini ya bati siyo kukaa chini ya miti au hovyo hovyo kitu kinachofanya ajira zao kuwa za watu wengi wahuni.
Mmmm stendi zote za mabasi ya daladala zimeezekwa vibanda ? Abiria mbona hukaa juani na mvua yao wakisubiri .Cha kwanza wasajiliwe sehemu zingine utakuta bodaboda wenyewe wamejijengea Banda la kukaa wakisubiri abiria kwa kujichangisha wenyewe

Sisi abiria stendi nyingi za daladala Wala hazina pa Sisi kukaa bandani

Ungeongelea majengo ya abiria walau ningeelewa
 
Pale mkuu wa mkoa anapokua kipaumbele chake ni bodaboda na machinga!!!! Inapendezaaaa
 
Basi wapewe leseni za kusafirisha mizigo.
... vyombo vya kusafirisha mizigo vina specs zake! Kama bodaboda na bajaji zina-meet vigezo well and good!
 
Wazo zuri , linaweza punguza uhalifu wa boda boda kwa abilia
 
Back
Top Bottom