Habari. Katika shughuli zangu za kiujasiriamali nilihitaji kwenda kununua dollar 20 ktk bureau de change moja hapa mjini Dar. Wakanipa dollar 20 ambayo baada ya kufika home nikagundua kuwa ilikuwa feki. Baada ya siku kadhaa nikaamua niirudishe pale ili wajue kuwa walinipa dola feki. Kufika pale nikakuta yule muhudumu aliyenihudumia siku kadhaa nyuma hayupo nikaamua kuibadilisha kwa yule niliyemkuta. Cha kushangaza hata hakuiangalia vizuri akanipa hela ya kibongo.
Ishu yangu ni kuwa ni hatari kwa sisi wajasiriamali maana je km ningeipeleka benki ingetambuliwa na ingekuwa ni tatizo kwangu. Je wajasiriamali tunajilindaje na dola feki, ila swali la msingi je bureau de change za hapa mjini wanachunguza kama dola wanazoletewa pale ni feki au la? experience zenu ni vipi?